YALEYALE: BRAZIL YATUPWA NJE COPA AMERIKA
Muuaji wa Brazil Derlis Gonzalez |
Kama ilivyotokea mwaka 2011 wakati Brazil wanakubali kichapo cha penati 2-0 dhidi ya Paraguay ndivyo ilivyotokea tena mwaka huu usiku wa kuamikia leo baada ya Timu ya Taifa ya Brazil kutupwa nje ya michuano ya Copa America baada ya kutolewa tena na Paraguay kwa mikwaju ya penati 4-3.
Brazil walitoka kwa mikwaju hiyo ya penati baada ya mechi hiyo ya Robo fainali kumaliza dakika 90 mabao yakiwa 1-1 ndipo mikwaju ya penati ilipokuja kutumika kuwapa Paraguay ushindi wa pili mfululizo katika hatua ya Robo fainali kama ilivyokua mwaka 2011.
Katika mchezo wenyewe Brazil walitangulia kupata bao kupitia kwa Robinho Dakika ya 15 alipounganisha Krosi safi ya Dani Alves kabla ya Paraguay kusawazisha kwa Penati ya Derlis González Dakika ya 72 baada ya Silva kuunawa Mpira ndani ya eneo la hatari.
Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na ndipo ikaja changamoto ya Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Kwa matokeo hayo Paraguay imetinga hatua ya Nusu fainali na itacheza na Argentina siku ya Jumanne ikitanguliwa na nusu fainal ya kwanza Jumatatu ambapo wenyeji Chile wataialika Peru huku fainali ikipangwa kucheza Jumamosi ijayo.
No comments