TAIFA STARS KUANZA UPYA SIO UJINGA
Awali ya yote nikupe pole mtanzania mwenye mapenzi ya dhati na timu yetu ya taifa kwa vipigo vikali "visivyo vya kubahatisha" kila kukicha.
KWA NINI SISI KILA SIKU? mfumo wa Soka? Uongozi mbovu? Bahati? Maandalizi duni? Najiuliza sipati jibu lakini hebu tuangalie hali halisi ya kikosi cha timu ya taifa kuanzia huduma hadi kiwango halisi kiwango.
Ni ukweli usiopingika kuhusiana na uchaguzi wa kikosi chetu cha timu ya taifa kugubikwa na lundo la wachezaji wa akiba katika vilabu vyao na kupewa kipaumbele katika timu ya taifa. Amir Kiemba,Kelvin Friday, John Bocco, Deogratius Munishi,Erasto Nyoni na wengineo wameendelea kuaminiwa na mwalimu angali hawana namba ya kudumu vilabuni kwao.
Mashindano ya CHAN yamebeba taswira ya wanaotamba katika ligi ya ndani je kwa stars yetu hii ni kweli?
Hassan kessy ,Juma Abdul, Malimi Busungu Mohammed Hussein "Tshabalala", Rashid Mandawa, Salum Telela, Hassan Mwasapili,Deus Kaseke hata Ally Mstafa "barthez" ni baadhi ya nyota kadhaa waliotamba musimu huu lakini wamekosa bahati hata ya kucheza mechi za CHAN
Yangekuwa maamuzi yangu ningemkabidhi kocha mzawa timu kwa ajili ya mashindano haya ya ndani. Martin Nooj ameshindwa kutupa imani watanzania juu ya uwezo wake.Hongera TFF kwa kumtimua ila msiishie hapo nanyi mjitathimini mapungufu katka nafasi yenu.. wakati wa mabadiliko tusiishie kubadili jezi tu ya timu ya taifa na kutumia gharama za ajabu za kambi isiyo kuwa na manufaa huku zikiharibu programu za vilabu bila faida yoyote.
NAIPENDA TANZANIA
AhsanteniVedasto Mfilinge
0659812805
No comments