MAJANGA : TUISAHAU PARMA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA
Mwaka 1999 wakati Man United wanabeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu ya FC Parma ikiwa katika ubora wake ilinyakua ubingwa wa Europa Cup
Ni moja kati ya timu za Italia zilizotingisha ulimwengu wa soka na miaka ya 2000 ilikuwa maarufu sana kwa kuwa na wachezaji waliokuwa na viwango vya juu...
Wakati huo waliwahi kuwa na watu kama viungo Ariel Ortega na Juan Sebastian Veron bila kumsahau mshambuliaji mwingine muargentina Hernan Crespo na walikuwa na beki mkali mfaransa Lilian Thuram,Fabio Canavaro bila kumsahau kipa wa kimataifa wa Italia Gianluigi Buffon ambaye bado anakipiga katika klabu ya Juventus hivi sasa...
Baada ya miaka 16 Parma ikishiriki Ligi kuu Nchini Italia Serie A yani msimu uliopita imejikuta ikikumbwa na hali mbaya kipesa huku wakikaribia kupokonywa pointi na kushushwa daraja... Ilifikia hatua hata maji ya kunywa mazoeni ni shida. Lakini walipona pona na kuendelea kuwepo kwenye ligi hadi msimu ukaisha.
Lakini baada ya msimu kumalizika hali ilizidi kua mbaya huku wakihaha kutafuta mtu au Kampuni ya kuwanusuru na balaa linalowakabili wakiwa tayari wameshuka daraja kutoka ligi kuu mpaka ligi daraja la kwanza maarufu kama SERIE B na baada ya juhudi zote hizo kushindikana siku ya leo tarehe 22 Juni 2015 Parma FC Imetangazwa rasmi kufilisika hivyo kushushwa daraja hadi ligi daraja la nne nchini Italia maarufu kama Serie D.
Ligi ambayo haina udhamini wowote na wachezaji sio wa kulipwa bali hucheza kwa ridhaa tu na hii ni kutokana na hilo deni ambalo thamani yake inafikia Euro milioni 22.6 na kwakushushwa huko ina maana deni hilo litaweza kulipwa kutokana na mali za klabu.
No comments