KARIBU FUNDI FIRMINO, KARIBU UFURAHIE UBINGWA
Njia ya kipofu ni mti wake.. Akiweza kuushika vizuri basi haina haja ya kumshika mkono. Mwaka jana siku tatu baada ya fainali za kombe la dunia kocha wa Manchester United Louis Van Gaal alikaa na vyombo vya habari vya Uingereza na kusema kwa sasa hatokua 'busy' kushughulika na usajili na badala yake atawachunguza wachezaji kwanza kisha atawapa nafasi kuonesha uwezo wao, kama kutatokea ulazima wa kusajili atatsajili ila kama watafanya vizuri basi kulikua hakuna haja au ulazima wa kusajili.
Timu ilianza maandalizi ya msimu na baada ya kurudi
kujiandaa kwa Ligi tukaona rungu au panga karibu wachezaji 8 kutemwa.
Rungu liliendelea mpaka sasa kufika idadi ya wachezaji 13 ndani ya msimu
wake wa kwanza. Hii yote ilitokana na falsafa za kocha ikiwemo kupata
wachezaji sahihi watakaoendana na mfumo atakaokuwa akiutumia. Tumeona
Van Gaal akitumia mifumo tofauti tangu alipoingia United lakini mfumo
wake wa kwanza alioupendelea ulikua ni 3-5-2. Nyuma mabeki watatu kisha
kunakuwa na wachezaji watano ambao wawili kati yao wanacheza winga ya
kupanda na kushuka.
Mfumo huu ulikua ukiwafanya United
kutawala sana mpira bila kutengeneza nafasi za kufunga.. Fowadi mbili za
mbele zilikua zikilazimiswa kujitanua pindi wanaposhambuliwa ili "wing
back" zirudi nyuma kusaidia mabeki watatu. Wakipata mpira na kuanza
kushambulia wanajikuta wanaanza kujipanga upya kitu kinachsababisha
viungo kuanza kukaa na mpira na kuanza kupasiana kusiko na mwelekeo.
Haukua mfumo mbaya na pia haukua mfumo mzuri kwetu pindi tunapofungwa
mapema.
Ilikua ni jukumu la Kocha na benchi lake la ufundi
kutuletea plan B ya mfumo lakini pia shukrani ziwaendee mashabiki kwa
makelele yao ya "Atttack Attack" yalisaidia kuubadilisha ubongo wa Louis
Van Gaal ktk fikra zake na kubadili muelekeo wa Jahazi lake. Ndipo
alipokuja na mfumo wa 4-1-4-1 au 4-1-3-1-1 na 4-4-2 kivuli ikiwemo na
4-3-3 kulingana na mchezo unvyokwenda.
Kama unakumbuka kuna mechi kabla
ya mapumziko wakiwa kwenye benchi LVG aligeuka nyuma kisha kumwambia
Fellain maneno ya kwenda kupigana na vita kwa ajili ya kuikomboa jezi
aliyoivaa. Ndio kipindi hicho alichomwambia Fellain sasa ni wakati wako
wa kuonesha kile kitu kilichokufanya nikamuuza Shinji Kagawa na
kukubakisha wewe.
Robin Van Persie aliumia.. Na ikawa njia
pekee ya kusimamisha foward mmoja mbele huku Fellain akisimama kama
daraja la mto Ruvu kuwaunganisha wakazi wa Chalinze na wakazi wa Kibaha.
Sehemu hii ambalo napenda kuita kiini cha shimo ndio sehemu ambayo
klabu nyingi zinapenda kutumia.. Central Attacking mildfielder kifupi
(No.10). Hii ndio sehemu ambayo Fellain alikua akicheza Everton na
Belgium. Sehemu hii Moyes alishindwa kuitumia hasa baada ya uwepo wa
Shinji Kagawa na baadae Juan Mata kitu kilichompelekea akashindwa
kumtumia vizuri Maroune Fellain japo walitoka wote sehemu moja.
Kwa
mfumo wa 4-1-4-1 au 4-1-3-1-1 mara nyingi Fellain alikua akicheza nyuma
ya Wayne Rooney kisha A.Young, Mata, Herrera, Blind/Carrick wakijidai
sehemu ya kati. Fellain anaposimama nyuma ya Rooney anakua kama
attacking mildfielder anayewaunganisha wakazi wa mbele ambaye ni Rooney
pamoja na wakazi wa nyuma yake amabao ni viungo wa kati. Kwetu kwa
bahati mbaya alikua si mtu wa kasi au mwenye manjonjo kama ya
Zinadine Zidane ila Fellain alikua ball controler mwenye uwezo wa
kutumia mwili wake vizuri kuunganisha mbele na nyuma.
SWALI: KWA NINI FELLAIN??
Shinji
Kagawa, Juan Mata, Wayne Rooney, Adnan Januzaj, Andrea Perreira, pamoja
na Fellain wote kwa pamoja waliweza kucheza kama central attacking
mildfielder. But why Fellain??
Ukijaribu kupitia mwanzo hasa
kauli ya Louis Van Gaal alisema anataka kuwapa nafasi wachezaji kwanza
kuonsha vipaji vyao ndio maana sikushangaa kuuzwa kwa Shinji Kagawa na
kubadilishwa namba kwa Juan Mata kama namba 7 kivuli. Kuumia kwa Robin
ilibidi Rooney aende mbele kisha Fellain asimame nyuma yake. Sehemu hii
ilikua muhimu na mtu pekee aliyehimudu basi alikua ni Fellain. Januzaj
alimuweka kama winga na Perreira bado ana miaka 18 hivyo hajakomaa vzr
kusimama kama mchezaji tegemeo.
KAULI;
Attacking
mildfielder mbona tunao wengi?? Kauli hizi mashabiki tunapenda sana
kuzitumia hasa tunapojaribu kukipanga kikosi chetu. Lakini ukweli kwa
sasa timu yetu ina attacking mildfielder mmoja tu ambaye ni Fellain.
Ander Herrera yeye ni central mildfielder mwenye uwezo wa kuaattack
wakati Blind na Carrick wao ni holding mildfielder. Alibaki Juan Mata
pekee ambaye kwa mfumo mpya wa LVG amebaki kuwekwa kama namba 7 kivuli
yenye uwezo wa kusaidia zaidi kiungo kuliko kwenda wide wing. Kivuli cha
Mata ndio kinachomsaidia Valencia kupanda kushambulia huku Mata akitoka
7 na kuingia kati.
Nilitaka kuanza kuzungumzia hali halisi ya
kikosi chetu, mfumo wa kisasa unaotumiwa na klabu nyingi kwa sasa
pamoja na usajili mpya kwa msimu ujao ili tupate kujua kiundani zaidi
nini tunahitaji kuliko kukaa na kuanza kusikitika au kunung"unika kwa
nini fulani hao tunao wengi.
Barcelona, Real Madrid, Bayern
Munich, Chelsea, Man City pamoja na Arsenal.. Klabu zote hizi kubwa kwa
mfumo wanaotumia mbele wanasimamisha foward mmoja. Barca atasimama
Suarez peke yake, Madrid atasimama Benzema peke yake, kisha Lewandowisk,
Diego Costa, Aguero pamoja na Giroud ni mafoward pekee ktk klabu zao
wanaosimama peke yao mbele kwa neno lingine "alone striker". Hawa
siku zote ulindwa na attacking mildfielder kama Lionel Messi kwa barca,
James Rodrigez kwa Madrid, Muller kwa Bayern, Oscar kwa Chelsea, Silva
kwa City pamoja na Santi Carzola au Mesut Ozil kwa upande wa Arsenal.
JE UMEWAHI KUJIULIZA MFUMO MPYA WA VAN GAAL??
Wengi
tunaweza kushindwa lakini kwa kuangalia falsafa zake alizokuja nazo hasa
baada ya kuikacha ule mfumo wa 3-5-2 na kuja na huu wa 4-1-4-1 utagundua
mfumo wake mpya ni wa kusimamisha foward mmoja mbele ambaye bila shaka
ni captain Wayne Rooney. Kwa mfumo huu ndipo tunapohitaji attacking
mildfielder mwenye uwezo wa hali ya juu kama wenzetu.
Lengo la
haya yote ni kutaka kumzungumzia kipaji kutoka taifa la Brazil ambaye
anatokea ktk klabu ya Hoffeinheim iliyopo Bundesliga Ujerumani, Roberto
Firmino. Huyu ndie mrithi sahihi na mchezaji tunayemuhitaji kwa sasa.
Ni attacking mildfielder mwenye uwezo wa hali ya juu ya kukaa na mipira,
kupiga chenga, kutoa pasi za uhakika za mabao na kubwa kuliko yote ana
uwezo pia wa kufunga. Brazili kwa miaka mingi imekosa namba 9 mzuri wa
kufunga but kwa ujio wa Neymar pembeni na Oscar nyuma yao mara nyingi
Dunga anapenda kumtumia Firmino kama namba 9 kivuli hasa kutokana na
uwezo wake wa kuunganisha daraja la mto Ruvu kati ya wakazi wa chalinze
na kibaha..
Habari zilizopo kwa sasa ni kuwa Wakala wake
ambaye ndio amesimamia maisha yake ya soka jana amewathibitishia vyombo
vya habari kuwa Roberto Firmino ataondoka Hoffeinheim na kwenda kucheza
soka lake Uingereza. Kitu pekee alichoficha ni klabu atakayokwenda japo
ukweli inasemekana anakwenda kujiunga na klabu ya Manchester United
kutokana na taarifa nyingi na vyanzo vingi kuelezea hivyo. Kwani hakuna
klabu ya uingereza ilionesha nia kwa kufika dau lake zaidi ya Manchester
United.
Uwepo wa Firmino utakua kama mbadala wa Fellain hasa
ukizingatia tuna wigo mpana wa mashindano mengi kwa msimu ujao. Pia
Fellain kwa sasa ni majeruhi jambo liliompelekea ata kukosa kwa mechi za
kufuzu zinazoendelea kwa sasa ktk timu yake ya taifa. Roberto Firmino
kwa sasa ndie mchezaji mwenye kipaji anayekuja kwa kasi nchini Brazil
pamoja na klabu yake ya Hoffenheim iliyopo Ujerumani. Ana umri wa miaka
23 na kwa sasa yupo nchini Chile akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil
akiiwakilisha michuano ya Copa America. Ni aina ya wachezaji kama Kevin
de Brune au Kaka wa Ac Milan pamoja na aina ya wachezaji niliyowataja
hapo juu wenye uwezo wa kuwaunganisha viungo na washambuliaji..
Attacking mildfielder wanaocheza karibu na kiini cha shimo.
Namaliza
kwa kusema mashabiki wa Manchester tusiwe na mchecheto wa kusema namba
hiyo tunao wengi, muhimu tuangalie vizuri kwa mapana kikosi chetu.
Tusiwe na haraka ya kusema kiungo mkabaji au beki kwani Van Gaal anajua
mengi kuliko sisi. Kama una kumbukumbu ligi ilivyoisha alisema mwenyewe
kwamba Our first priority ni difensive mildfielder ambaye atasaidiana na
Michael Carrick lakini cha ajabu unaweza kushangaa amemsajili Memphis
Depay na sasa Roberto Firmino. Hivyo suala la kiungo mkabaji atamsajili
tusiwe na wasi muhimu nilichopenda ni kuwawahi hawa wachezaji wa kuziba
mashimo na kufanya msimu ujao tuwe shots on target nyingi
zitakazotufanya kuwafunga wapinzani. Louis Van Gaal kipofu aliyepata
fimbo yake nzuri kwa sasa ameijua njia tumuache ajiongoze mwenyewe.
Welcome fundi Roberto Firmino
Na David Peter Herera
No comments