JULIO AZIPONDA TUZO ZA LIGI KUU TANZANIA BARA

Kocha Mkuu wa timu iliyopanda daraja ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu maarufu kama Julio ameibuka na kuzipondea tuzo zilizotolewa na bodi ya Ligi kuu Tanzania bara wakishirikiana na Mdhamini mkuu Kampuni ya Vodacom.

Akizungumza na WAPENDA SOKA weekendi iliyopita Julio amesema tuzo hizo hazikufata welesi hasa katika kipengele cha kocha bora wa msimu ambayo ilienda kwa Aliyekua kocha wa Prisons Mbwana Makata.

Julio amesema yeye ni Bora kuliko Makata na hajui kitu gani walichozingatia waandaaji kumpa Mbwana Makata wakati yeye alikua juu yake, Ameendelea kusema "Mimi na Mbwana wote tulikua ligi daraja la Kwanza tena kundi moja kundi ambalo mimi na timu yangu ya Mwadui tulifanikiwa kumaliza washindi wa kwanza katika kundi lile na hatimaye kuchukua ubingwa wa Ligi daraja la Kwanza lakini mwenzangu yeye alishika nafasi ya tatu akiwa na JKT Oljoro ya Arusha"

Aliendelea kusema "Baadae wote tukafanikiwa kupata timu za kuzifundisha katika ligi kuu hatua ya lala salama na wote tukipewa timu ambazo zilikua katika janga la kushuka daraja bahati nzuri mimi nikajitahidi kuinyanyua Coastal Union na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tano tukilingana na Mbeya city kwa point lakini Mbwana Makata na Prisons walimaliza kwa kushika nafasi ya 11 hapo nani ni bora?"

Tuzo za Washindi wa Ligi kuu ya Vodacom zilitolewa Ijumaa iliyopita huku zikizua maswali kwa washindi waliopatikana hasa Kocha bora na kipa bora ambayo ilichukuliwa na Shaban Kado aliyekua akidakia Coastal union.

No comments

Powered by Blogger.