FAIDA YA IDADI YA WACHEZAJI WAKIGENI NA MAENDELEO YA TIMU YA TAIFAA



Mbali na kuwa sehemu ya kuleta umoja,Amani katika jamii, kwasasa tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu imekuwa sehemu ya kitega uchumi kwa watu wengi, hata serikali nyingi zinapata baadhi ya pato kutoka katika tozo ya kodi inayokusanywa katika vilabu, viingilio vya mechi za timu ha taifa na kupelekea nchi nyingi kujikita katika kuendeleza michezo hasa mpira wa miguu kuanzia ngazi ya vilabu na timu ya taifa lengo ni kuwa miongoni mwa nchi zenye mafanikio makubwa kisoka na Tanzania ni moja ya nchi hizi.



Kuna faida nyingi endapo nchi husika ikifanikiwa kuimarisha mchezo huu,moja wapo ni kuwa na ligi bora, kuvutia wawekezaji, kuwa na timu bora kuanzia ngazi ya vilabu na timu ya taifa,pia  kuvutia wachezaji wa kigeni kitu ambacho kinaweza itangaza ligi katika tasinia ya mpira wa miguu ulimwenguni.

Wiki kadhaa zilizopita ,baadhi ya vilabu nchini Tanzania vilituma ombi kwa TFF la kuongezewa wachezaji wa kigeni kutoka idadi ya sasa ya wachezaji 5 na ifike adi 10, sababu kuu ni kutaka kuwa washindani katika michuano ya kimataifa hususani klabu bingwa na kombe la shirikisho kwani huko hukutana na vilabu vyenye wachezaji wazuri, wakimataifa na hivyo kupelekea kutolewa mapema.

Kitu ambacho TFF,kupitia  kamati yake ya utendaji wameafiki ni ombi hil0  na kutangaza kila klabu itaruhusiwa kusaji wachezaji 7 wa kigeni na klabu husika inaweza kuwatumia wachezaji wote saba katika mechi moja.Mbali na hill,TFF pia imeweka ada kwa kila mchezaji atakayesajiliwa kwa ajiri ya kuhimarisha timu za vijana.

Tukianza na suala la ada, hapa TFF imeweka kiwango kikubwa sana na pengine kingeondelewa au kupunguza toka dola 2000 adi 500 ili  kutoa fursa hata kwa vilabu kama Ndanda, Toto Africans kumudu tozo hii kwa minajili ya kuendeleza mpira hapa nchini. Kwani ni dhahiri kabsa tozo hii ni  kubwa na klabu chache zenye vipato vikubwa kidogo ndo zitakazoweza kumudu tozo hii, na pia kwa kiwngo hiki cha 2000 klabu zitakuwa hazina faida kwani yote itakuwa ikiishia kulipa gharama za wachezaji hawa.


Tukirejea katika suala la idadi ya wachezaji wa kigeni ningependa kuliweka suala hili Kama mpango wa muda mfupi( short term plan) ambazo ni Kama njia kuelekea mpango endelevu( Long term plan) za kuhimarisha ligi, vilabu na timu ya taifa ya Tanzania kupitia uwekezaji katika kujenga vituo maalumu vya mpira Kama nchi nza wenzetu zifanyavyo.

Kwa kifupi tu, faida za mpango huu za kuwa na idadi ya wachezaji wa kigeni ipo kwa ngazi ya vilabu na si timu ya taifa ambayo ndo kiunganishi cha watu wa taifa husika kwani timu ya taifa inapocheza watu wote kama vile wapinzani wa jadi huwa kitu kimoja na ndio maana tunapofanya vibaya huitwa timu ya taifa ya Tanzania na si klabu ya Tanzania hii ni kwasababu imeundwa na wachezaji wazawa kutoka sehemu mbali mbali mwa Tanzania. Hivyo kuwa na vilabu vinavyofanya vizuri lakini timu ya taifa ni mbovu ni upuuzi.


Moja ya faida zinazotokana na mpango huu ambao mimi nauita kama mpango mfupi(short term plan) kuelekea katika mpango mrefu(long term plan) ni  utawezesha vilabu vyetu vinavyoshirika michuano ya kimataifa kuwa shindani katika michuano hiyo na kunaweza palekea kufika hatua nzuri Kama fainali Kama baadhi ya vilabu vinavyowekeza katika watu ili wachezaji hao waipeleke klabu hivyo fainali.

Pia, Kukuza ujuzi kwa wachezaji wazawa kupitia wachezaji wa kigeni. Ujuzi huu wataupata kwa kubadilishana mawazo ya kipi mchazjai unatakiwa ufanye ili na wewe ukacheze soka la kulipwa huko nje ya nchi, pia kutoa changamoto kwa wachezaji wazawa na kuonesha juhudi katika kupigania namba ndani ya vilabu vyao.


Suala hili la wachezaji wakigeni, nimeliweka katika mpango mfupi kwasababu faida yake ipo katika vilabu tu kama nilivyosema hapo juu na si katika timu ya taifa. Hii ni kutokana na sababu kadhaa moja wapo ni wachezaji wazawa kutokupata nafasi za kuonesha vipaji vyao, mathalani klabu za simba, Yanga na Azam ndo vilabu pekee vinavyotoa wachezaji wengi katika timu ya taifa, na vilabu hivi ndivyo vinashiriki michuano ya kimataifa kwa kiasi kikubwa.


Swali Je, ikiwa kama vilabu hivi vimepewa ruhusa ya kuwa na wachezaji hawa na kuwatumia wote katika mchezo mmoja kunauwezakano wa kukuta wachezaji wa nyumba ni hao 4, tena utakuta ni walinzi tu hivyo kutoa nafasi kwa wachezaji wa kimataifa hususani wafungaji, viuongo kuendelea kupata uzoefu mkubwa na hivyo kuzisaidia timu zao za taifa na timu yetu kuonekana haina wafungaji kumbe hawajapewa nafasi ya kutumika ipasavyo.


Unaweza jiuliza mbona nchi za magharibi zimeruhusu idadi wengi ya wachezaji, mfano uhisipania imeruhusu klabu zao kuwa na wachezaji wengi, jibu ni kwamba nchi hizi zinawachezaji wengi wanaocheza ligi za kubwa za nje tofauti na kwa Tanzania ambayo kila mwaka tunawaita wale wale wachezaji wetu 4, hii ni kusema idadi ya wachezaji wanaocheza nje katika ligi za ushindani ni wachache kulinganisha na nchi nyingine ambazo inakuwa rahisi kwa makocha kuita timu ya taifa kwani anaona na kusikia kiwango cha wachezaji hao.


Hata Tanzania ingekuwa na idadi kubwa ya wachezaji wazawa wanaocheza nje ya nchi katika ligi yenye ushindani, tukubali kuwa hata na wachezaji 14 wa kigeni kama ilivyofanya nchi ya uturuki mapema mwaka huu kupitia raisi wa shirikisho la Mpira wa miguu  wa nchi hiyo (Turkish football federation)TFF, Bwana Yıldırım Demirören alitangaza mabadiliko ayo kuanza kutumika katika msimu wa mwaka 2015/2016, kitu ambacho ni hatari kwa maendeleo ya soka la nchi kama Tanzania ambayo inapigania kujikwamua toka chini na kuwa katika nchi zilipiga hatua kisoka.


Mathalani nchini Russia,  kuna mpango wa kupunguza wachezaji wa kigeni lengo ni kutoa nafasi kwa wachezaj wa rusia ili wapate uzoefu kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia 2018 lengo ni kuwa na vijana watakaounda timu imara itakayokuwa ni timu shidani na si washiriki.


Hivyo, katika malengo marefu yenye tija kwa timu ya taifa,  baada ya serikali, TFF na vilabu kufanikisha zoezi la kuwa na vituo maalumu vya mpira, ndo utakuwa mda sahihi kwa TFF kutazama upya sheria hii lengo ni kuwapa nafasi vijana wetu kuonyesha vipaji vyao na pia kuweza kunyanyua kiwango cha timu ya taifa.kwani kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni ni faida kwa vilabu na timu za taifa za nchi wanazotoka na si kwa maendeeleo ya timu yetu ya taifa.

... Imeandaliwa na Omary Sadick 

No comments

Powered by Blogger.