YANGA YAMALIZA LIGI KWA KICHAPO. MASAU BWIRE BYE BYE LIGI KUU



Ligi kuu ya Soka ya Tanzania Bara imefikia tamati leo baada ya kuchezwa michezo 7 ambayo iliziweka dimbani timu zote 14.

Mechi za leo zilikua ni za kutafuta timu zipi zitashuka daraja baada ya timu za juu kujulikana tayari kabla ya mechi za leo.

Mabingwa wapya wa ligi hiyo Yanga walikua ugenini kule Mtwara wakicheza na Ndanda FC na kutoka katika uwanja wa Nangwanda Yanga walikubali kichapo cha bao 1-0 matokeo ambayo yamewapa tiketi ya kubaki ligi kuu Ndanda FC.

Jijini Dar Es Salaam Simba waliinyuka JKT Ruvu bao 2-1 Wakati Azam FC wao walilazimishwa sare ya bila kufungana na Mgambo JKT matokeo ambayo hayabadilishi kitu kwa Azam FC na Simba lakini yamewapa nafasi Mgambo kubaki katika ligi kuu.

Mjini Shinyanga kulikua na msiba kwa Masau Bwire ambaye ni msemaji wa Ruvu Shooting kwani akiwa na timu yake hiyo alikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Stand United matokeo ambayo yamewashusha Ruvu Shooting kwa tofauti ya magoli.

Jijini Mbeya klabu ya Mbeya City iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro na kuishusha timu hiyo ya jeshi la Polisi.

Mtibwa wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Coastal Union. Kagera Sugar walilazimishwa sare na Prisons katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza.

No comments

Powered by Blogger.