NORWICH WARUDI LIGI KUU ENGLAND


Baada ya kushuka misimu miwili iliyopita hatimaye Norwich City wamerejekatika ligi kuu nchini England baada ya kuwabamiza Middlesbrough bao 2-0 katika mchezo wa fainali ya "play off" kupata timu ya tatu itakayoungana na timu mbili ambazo zimeshapanda daraja Bournemouth na Watford.

Norwich ambao walikamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu walipata magoli yao kupitia kwa Cameroun Jerome na Nathan Redmond magoli ambayo yanawarudisha tena kucheza katika viwanja vikubwa na maarufu kama Old Trafford, Emirates na Anfield.

 Norwich inafundishwa na kocha mwenye umri mdogo kabisa Alex Neil mwenye miaka 33 tu iliweza kushinda mechi hiyo katika uwanj
 Wa Wembleh ambao leo ulijaa kwa takribani mashabiki 85,000 na kujishindia kitita paundi milioni 120 kwa kushindamechi hiyo


No comments

Powered by Blogger.