MBIO ZA ARSENAL NA MAN UNITED KATIKA KUPIGANIA NAFASI YA TATU EPL


... Baada ya Arsenal kutoka sare jana dhidi ya Sunderland, Imefikisha pointi 72 ikiwa katika nafasi ya Tatu katika msimamo wa Ligi kuu nchini England wakati huo huo Man United wao wana pointi 69 baada ya kulazimishwa sare Jumapili iliyopita dhidi ya Arsenal na timu zote hizi zimebakiza mchezo mmoja

Arsenal watakua nyumbani wakicheza na West Brom wakati Man United wao watakua ugenini kucheza na timu inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Hull City ambayo kama itafungwa itashuka daraja.

Swali kubwa tunalolipata hapa je MAN UNITED INAWEZA KUSHIKA NAFASI YA 3?

Kwa kifupi ili Man United ishike nafasi ya 3 kwanza itatakiwa kushinda mechi yake ya mwisho na kuombea Arsenal ifungwe na West Brom bao nyingi.

Wakati Arsenal wao wanahitaji sare tu kushika nafasi ya 3 kikamilifu hii ni kama United ikishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Hull City lakini kama itatoka sare au kufungwa basi Arsenal iko katika nafasi ya Tatu.

Arsenal na Man United zimecheza mechi 37 kila moja mpaka sasa Arsenal imeshinda mechi 21 United Ikishinda mechi 20. Timu zote mbili hizo zimetoka sare mara 9, Arsenal ikipoteza mara 7 na united imepoteza mara 8.
Kwa Upande wa Magoli Arsenal imefunga magoli 67 huku United ikifunga Magoli 62 na Arsenal imeruhusu wavu wake kutikiswa mara 35 huku United wakiruhusu Kufungwa mara 37.

Katika huo mchakato hapo Juu Arsenal inatofauti kati ya magoli ya kufunga na kufungwa 32 wakati Man United wao wana tofauti ya magoli 25 hivyo ili United Ishike nafasi ya Tatu itabidi ishinde bao 8-0 katika mechi yake ya mwisho na kuombea Arsenal ifungwe.

NAFASI YA TIMU ZITAKAZOCHEZA NA ARSENAL NA UNITED


West Bromwich Albion ikishika nafasi ya 13 na pointi zake 44 haina cha kupoteza itasafiri mpaka London kuikabili Arsenal ikiwa haina presha yoyote ya matokeo ya mechi hiyo ya mwisho.

Kwa Upande wao HULL CITY mambo ni tofauti mno kwani wanahitaji ushindi kuliko kitu kingine chochote. Wanashika nafasi ya 18 wakiwa na pointi 34 juu yao wako Newcastle ambao wana pointi 36 hivyo piga ua lazima washinde hiyo mechi ili wabaki ligi kuu zaidi ya hapo Hull City itashuka daraja kuungana na QPR na Burnley ambao tayari wameshashuka daraja.

NINI UTABIRI WAKO HAPA KUHUSU TIMU YA TATU NA ILE ITAKAYOSHUKA DARAJA?

1 comment:

  1. Arsena akifungwa mbili na man ashinde tano watafanana kila kitu. Hapo ni ngumu Sana hii

    ReplyDelete

Powered by Blogger.