INSIDE UNITED ~ WAYNE ROONEY AWEKA REKODI YA AINA YAKE ENGLAND
Baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu sasa ile segment pendwa ya mashabiki wa timu ya manchester United imerudi na leo katika INSIDE UNITED tunamwangazia WAYNE ROONEY.
Baada ya kumalizika msimu wa ligi kuu nchini England, Nahodha wa Manchester United na Timu ya Taifa ya England Wayne Rooney amekua mchezaji wa kwanza katika Ligi kuu nchini England kufunga zaidi ya magoli 10 katika misimu 11 mfululizo iliyopita katika ligi hiyo.
Rooney amemaliza msimu huu akifunga mabao 12 katika ligi kuu akifunga jumla ya magoli 14 katika michuano yote na kumfanya mfungaji bora kabisa katika orodha ya wafungaji bora wa Man United msimu huu.
Mchezaji huyo aliyezaliwa katika kitongoji cha Croxteth jijini Liverpool England alizaliwa Oktoba 24,1985 na ameichezea Everton tangu mwaka 1996 akiwa katika vikosi vya vijana vya Everton kabla ya kupandishwa na kupewa nafasi katika timu ya wakubwa ya Everton na Aliyekua kocha Wa Everton David Moyes.
Akiwa na Everton ya wakubwa tangu mwaka 2002-2004 aliweza kufunga magoli 15 katika mechi 67 za ligi kuu Nchini England kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2004 kwa ada ya uhamisho ya paundi milion 25.6 ikiwa ni rekodi katika usajili wa mchezaji mwenye miaka chini ya 20 na kupachika mabao 170 katika mechi 340 za ligi kuu
Kwa Ujumla Rooney ameshafunga magoli 247 katika mechi 556 alizocheza katika maisha yake ya soka upande wa klabu kati ya hayo 17 akiifungia Everton na 230 akiifungia Man United.
Tangu alipojiunga na Man United Rooney hajawahi kuvukisha msimu hajafunga zaidi ya goli 10 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.
Ifuatayo ni orodha ya magoli kwa misimu 11 iliyopita kwa Wayne Rooney Tangu alipotua Man United.
2004-05 : 11
2005-06 : 16
2006-07 : 14
2007-08 : 12
2008-09 : 12
2009-10 : 26
2010-11 : 11
2011-12 : 27
2012-13 : 12
2013-14 : 17
2014-15 : 12
Kwa leo tuishie hapa tutamzungumzia vizuri Rooney siku nyingine ambapo tutaangalia rekodi zake na tuzo nyingi alizozishinda katika maisha yake ya soka.
No comments