HABARI 5 KALI ZA SOKA MCHANA HUU
... Natumai uko salama. Nimekuandalia baadhi ya habari za soka mpaka mchana huu
● Klabu ya Juventus imechukua kombe lake la pili msimu huu baada ya kuwafunga Lazio katika fainali ya kombe la Chama cha Soka nchini Italia (Copa Italia) kwa bao 2-1 magoli ya Juventus yakifungwa na beki Chielin na Mshambuliaji Alexandro Matri.
● Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas amepunguziwa adhabu yake ya kukosa mechi tatu na sasa atakosa mechi moja tu baada ya kupata kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mechi dhidi ya West Brom wikiend iliyopita ambapo mabingwa hao wapya wa England walipigwa bao 3-0.
● Kocha wa Borussia Dortmund Juggen Klopp ameanza mazungumzo na klabu ya Fernebahce ya Uturuki kutaka kupata kazi ya kuifundisha timu hiyo baada ya kutangaza kuondoka katika klabu ya Dortmund mwishoni mwa msimu huu.
● Magazeti mengi leo yameripoti kuwa Liverpool imekataa muda huo huo ilipopokea ofa ya Manchester United waliyoipeleka ili kumsajili Raheem Sterling ambaye kuna kila dalili ya mchezaji huyo kutaka kuondoka
● PSG Imeongoza katika orodha ya vilabu vinavyoongoza kulipa mishahara mikubwa kwa wachezaji ikiwa ni wastani ws malipo kwa wiki na hii ni orodha ya vilabu 10 bora vinavyoongoza kwa wastani wa malipo na kiasi cha pesa wanacholipa wachezaji wao kwa wiki.
1: Paris St Germain (£101,898)
2: Real Madrid (£96,933)
3: Manchester City (£96,445)
4: Barcelona (£90,675)
5: Los Angeles Dodgers (£89,999)
6: Manchester United (£89,988)
7: Bayern Munich (£85,935)
8: Chelsea (£83,713)
9: New York Yankees (£81,992)
10: Arsenal (£77,963)
... Endelea kutufatilia ili kupata mengi yahusuyo Soka
No comments