YANGA YAISHUSHIA COASTAL YA JULIO KIPIGO CHA BAO 8, TAMBWE APIGA 4

Tambwe na Msuva


Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Dar es Salaam Yaoung Africa (Yanga) jioni hii imeishusia kipigo cha mbwa Mwizi Coastal Union ya tanga kwa kuibamiza bao 8-0.

Yanga ambao ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Ilionyesha dhamiri ya dhati kuweza kuibuka na ushindi leo baada ya kuanza kwa mashambulizi ya nguvu ambayo yalizaa goli la kwanza kwa yanga likifungwa kwa Ustadi na Mshambuliaji aliyetemwa na Simba Amiss Tambwe kwa kichwa goli ambalo lilizaa mengine matatu kwa tambwe na kumfanya kuondoka na mpira katika mchezo huo kwa kufunga magoli manne peke yake.

Winga na Mshambuliaji aliye katika hali nzuri ya kufunga hivi sasa Simon Msuva yeye alitupia bao 2 peke yake wakati Salum Telela na Mliberia Kpah Sherman nao walitupia bao moja kila mmoja na kukamilisha ushindi wa bao 8-0 ushindi ambao pengine utavunja rekodi katika ligi kuu.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa wamezidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu kwa kufikisha pointi 43 na mechi ijayo Yanga itamenyana na Mbeya City Jijini Dar Jumapili hii.

++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.