THE GUNNING MACHINE: PAMBANO LA MSIMU KWA ARSENAL.


Na: Richard Leonce Chardboy.

Kama mpenda soka , una mambo mengi ya kufanya lakini kuna jambo ni lazima ulitimize leo. Si lingine ni kuelekeza macho na masikio yako Pale London ya Kaskazini katika dimba la Emirates ambapo kutakua na shughuli nzito.
Ni Sanchez dhidi ya Ivanovic, Giroud dhidi ya John Terry, huku Coquelin akijaribu kumzuia mtu ambaye alikua nahodha wa timu yake wakati yeye akiwa shuleni kujifunza soka, Ni Cesc Fabregas.

Ni aini ya mechi zenye utamu wa aina yake. Ni mechi inayowakutanisha tena mahasimu wawili wenye falsafa tofauti katika soka, Jose Mourinho na Arsene Wenger. Hawa hawapikiki wakaiva chungu kimoja.

Katika mchezo uliopita pale Stamford Bridge (darajani) walikunjana, walitamani wangekua peke yao ili wapigane lakini bahati nzuri kulikua na watu.

Ni mchezo ambao unawakutanisha watu wanaoshika nafasi ya pili wakiwakaribisha wanaoshika nafasi ya kwanza huku kila mmoja akiwa kwenye kiwango bora kabisa.

Arsene Wenger akijua kwamba tangu azaliwe hakuwahi kuifunga timu yoyote inayofundishwa na Mourinho, amesema mechi hiyo ya leo itahusu zaidi viwango vya timu hizo mbili na siyo historia kama wengi wanavyodhani.

Katika michezo sita iliyopita dhidi ya Chelsea, Arsenal wamefunga mara mbili tu huku Chelsea wakipata 'clean sheet' katika michezo minne.
Ni wazi, Arsenal wanaingia kama vibonde kwa Chelsea leo hii, wakihitaji ushindi kwa hali na mali ili wajiimarishe katika nafasi ya pili ambayo bado hawajajihakikishia hata kidogo.

Lakini pia ushindi utamaanisha kuisigolea Chelsea na pengine kufufua matumaini ya ubingwa.
Ushindi utaendeleza matokeo mazuri kwa Arsenal kwa mwaka huu wakiwa  wamevuna pointi nyingi zaidi ya timu yoyote tangu mwaka uanze.

Ni ushindi utakaomaanisha kwamba sasa Arsenal ni washindani wa kweli kwenye soka ya Uingereza, kumbuka ni Chelsea pekee ndio haijaonja kichapo cha Arsenal msimu huu katika timu vigogo vya soka.

Manchester United, Manchester City na Liverpool wote wamepokea vya kwao na ni jambo ambalo Arsenal walikua hawajafanya kwa misimu mingi iliyopita.
Ni wazi hili ni pambano la msimu.

Arsenal wanaweza kumkosa mlinzi wao Per Mertesacker ambae ni majeruhi, lakini pia Mikel Arteta na Alex Oxlade Chamberlain bado watasalia nje.

Ninayo haya hapa ambayo nataka uyajue tukielekea pambano hilo.

  •  Olivier Giroud amefunga mabao 10 katika michezo 12 iliyopita.
  •  Katika mwaka huu 2015, Chelsea wamecheza jumla ya michezo 20, na katika michezo hiyo yote wao ndio waliokua wa kwanza kupata goli.
  • Katika mwaka huu 2015 Arsenal wamekusanya pointi 33, ni nyingi zaidi ya timu yoyote katika ligi kuu ya England.
  •  2410 ni jumla ya dakika alizocheza Alexis Sanchez, akitengeneza nafasi 69. Akifunga magoli 14 na pasi za mwisho 8.


Asante.

No comments

Powered by Blogger.