THE GUNNING MACHINE: YAJUE HAYA MACHACHE KABLA YA PAMBANO DHIDI YA BURNLEY.


Na Richard Leonce Chardboy.


Arsenal wanakwenda ugenini kukwaana na Burnley leo hii April 11 kuendeleza kampeni yao ya kusaka pointi tatu ili wajiimarishe katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, tunasema "we are gunning for second". haya ni machache ambayo
nimeona uyajue wakati Arsenal wakielekea kwenye mchezo huo

Arsenal wamefunga magoli mengi ya mipira iliyotengwa, (set pieces) kuliko timu yoyote ua ligi kuu mpaka sasa wakiwa wamefunga magoli 20, hii ni tofauti na misimu kadhaa iliyopita ambapo Arsenal walikua hawatumii vema set pieces na badala yake walikua wakifungwa magoli ya aina hiyo kwa wingi.

Wawapo katika uwanja wao wa nyumbani, Burnley mo wavumilivu sana. Rekodi zinaonesha wamefungwa magoli matatu tu katika dakika 15 za mwisho
amnayo nimachache kiliko timu zoye za ligi kuu ziwapo katika uwanja wa nyumbani. hii inamaana ili kuwafunga Burnley unapaswa kufanya hivyo mapema.
Katika michezo 15 tu aliyocheza, Mesut 0zil amepiga pasi 838, akitengeneza jumla ya nafasi 39 na pasi za mwisho 5. kama nafasi zote 39 zingetumika vema basi Ozil angekua na pasi za mwisho 39.

Abou Diaby, Mikel Arteta, na Jack Wilshere wapo fit.
Methieu Debuchy bado hajapata nguvu ya ushindani na anaweza kuichezea timu ya vijana chini ya miaka 21.

Laurent Koscielny ana tatizo la paja lakini atafanyiwa vipimo mapema hii leo.
Alex Oxlade Chamberlain ataendelea kuwa nje walau kwa wiki mbili

No comments

Powered by Blogger.