SIMBA WATAKIWA KUWALIPA CHANONGO NA TAMBWE MAMILION YA PESA


Klabu ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015 vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo.

Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo
ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.

Amissi Tambwe vs Simba Sports Club

Mchezaji Amissi Tambwe aliwasilisha malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake
Desemba 15, 2014. Uamuzi wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014.

Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of Settlement).

Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014.

Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.

*********************

No comments

Powered by Blogger.