THE GUNNING MACHINE.
NI WEMBLEY TENA KUISAKA FAINALI.
Na Richard Leonce Chardboy.
Moja kati ya vitu muhimu vilivyosalia kwa Arsenal msimu huu, ni kushindania kombe la FA.
Arsenal wamefika hatua ya nusu fainali na jioni ya leo wakati Chelsea wakiwakaribisha Manchester United, wao watakua katika dimba kuu la Wembley kuisaka tiketi ya kucheza fainali mbele ya Reading.
Wakiwa katika mwendo mzuri wa matokeo, Arsenal watajivunia rekodi yao ya kushinda michezo nane mfululizo.
Ikiwa ni nusu fainali ya 10 ya Arsene Wenger kwenye kombe la FA, ataingia uwanjani akiwa na upana wa kutosha kwenye kikosi chake ambacho kitawakosa Alex Oxlade Chamberlain na Mikel Arteta pekee.
Wojciech Szczesny, golikipa ambae anaadhimisha miaka 25 ya kuzaliwa leo hii, anatarajiwa kusimama langoni, na hii ni nafasi kwake kuonesha upinzani kwa David Ospina ambaye ameipora namba yake katika kikosi cha kwanza cha washika mitutu hao.
Akizungumza juu ya hilo, Arsene Wenger amesema ana kawaidavya kutoa nafasi ukizingatia mabeki wake wamecheza mechi nyingi na Szczesny.
'yupo kwenye kiwango kizuri, alionesha kiwango katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Manchester United na hakuna sababu ya kutompa nafasi katika nusu fainali.'
Alisema Wenger.
Pia Jack Wilshere anaweza kutumika leo baada ya kupona majeraha yaliyokua yakimsumbua.
Aidha rekodi zinaonesha wachezaji 8 tofauti wa Arsenal wametikisa nyavu katika kombe la FA msimu huu, ikiwa ni wengi zaidi ya timu yoyote huku Olivier Giroud akitikisa mara mbili katika michezo mitatu aliyocheza.
Kwa upande wa Reading ambao hawana mwendo mzuri kwenye ligi daraja la kwanza, wao wana rekodi isiyokua ya kawaida sana katika kombe la FA msimu huu ambapo wameshuhudia wapinzani wao wakipata walau kadi moja nyekundu katika michezo mitatu kati ya minne iliyopita.
Hakika mashabiki wa Arsenal wataelekeza macho yao Wembley leo hii ili kuona kama timu yao itaelekea kutetea ubingwa walioupata msimu uliopita kwa bao la dakika za ziada la Aaron Ramsey.
katika hatua kama hii msimu uliopita Arsenal waliitoa Wigan kwa mikwaju ya Penati, shukrani kwa Lucasz Fabiaski ambaye leo pia anaadhimisha miaka 30 ya kuzaliwa kwake.
No comments