MECHI YA KAGERA VS SIMBA KUPIGWA KESHO JUMATATU 


.. Na Bab Chicharito (Shinyanga)

Pambano la ligi kuu Tanzania bara kati ya Kagera Sugar na Simba ya Dar es Salaam litafanyika jumatatu hii ya pasaka baada ya muafaka kufikiwa kati ya vilabu hivyo viwili na bodi ya ligi.

Pambano hilo lililopaswa kufanyika jana Jumamosi liliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha mjini Shinyanga na baadae ikasemekana kuwa mechi hiyo itachezwa Siku ya Jumatano lakini sasa muafaka umefikiwa kuwa mechi hiyo ichezwe kesho Jumatatu.

Simba iko tayari mkoani Shinyanga kwaajili ya pambano hilo lakini leo katika uwanja wa Kambarage litapigwa pambano kati ya wenyeji Stand United watakaocheza na Mtibwa Sugar.

No comments

Powered by Blogger.