LIGI KUU TANZANIA BARA : MTIBWA SUGAR KUISAHAULISHA AZAM UBINGWA LEO?





Na Edo Daniel Chibo, Dar Es Salaam

Kampeni za kuwania mbabe wa soka la Tanzania zinaendelea leo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara inayodhaminiwa na kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania.

Mabingwa watetezi Azam Fc ya jijini Dar Es Salaam itakua katika mashamba ya miwa ya Mtibwa ya mkoani Morogoro kuwakabili Mtibwa sugar pambano ambalo pengine litfuta ndoto za Azam FC kutetea ubingwa wao waliouchukua mwaka jana.

Azam FC Ina pointi 36 katika nafasi ya Pili itahitaji ushindi ili ijaribu kuifikia Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 43 baada ya mchezo uliopita kushindwa kupata matokeo na kuishia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City.

Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Stand United mjini Shinyanga wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na tahadhari kubwa huku wakijua kabisa ushindi kwao ni lazima ili kujikwamua na balaa la kushuka daraja kwani Mtibwa ina pointi 21 hivi sasa ikikamata nafasi ya 12 pointi ambazo ni sawa na za Polisi Morogoro wanaokamata mafasi ya 13

Katika mechi nyingine leo Ndanda FC ikiwa katika uwanja wake wa Nyumbani watawakaribisha Prisons ya mbeya ambayo inakamata nafasi ya mwisho katika msimamomchezo huo utapigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

JKT Ruvu wao watakua Katika dimba lao la Nyumbani Chamazi Complex kuwakabili Wachovu wa yanga timu ya Coastal Union toka Jijini tanga ambayo katikati ya wiki ilikubali kichapo cha bao 8-0 toka kwa vinara wa ligi hiyo Yanga.

Kagera Sugar baada ya kutembezewa kichapo na Mnyama Simba watabaki katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga kuwakabili Ruvu Shooting kutoka mkoani Pwani



+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.