LIGI KUU TANZANIA BARA - AZAM NA YANGA VIWANJANI JIONI HII
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea leo jumatano katika viwanja viwili jijini Dar es salaam, kwa vinara wa ligi hiyo Young Africans kuwakaribisha Coastal Union kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Uwanja wa Chamazi Complex, wenyeji timu ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, watawakaribsiha wagonga nyundo kutoka jijini Mbeya timu ya Mbeya City FC.
Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 40 Azam wanafatia wakiwa na pointi 36 huku Simba ikikamata nafasi ya 3 wakiwa na pointi 35.

No comments