KUELEKEA KATIKA MECHI YA ARSENAL VS CHELSEA....TUTIZAME HAYA MACHACHE
Usimchukie Mourinho na mbinu zake, katika wakati kama huu unahitaji Ulinzi ufanye kazi kuliko ushambuliaji, hii ni akili nyepesi na nzuri ambayo wengi uipuuza.
Coquelin vs Fabregas? Utamu upo hapa, akishinda huyu mfaransa Mashabiki hawatomkumbuka Fabregas, akishindwa Wenger atazungumzwa sana Leo, na majuto mengi.
Mesut Ozil.. Yupo katika kiwango ambacho hata mimi ningefurahia kucheza EPL mbele yake. Sidhani kama Mourinho atamhitaji sana Zouma leo, nadhani Ramires anaweza Kuwa option bora kuanza na Matic.
Bellerin vs Hazard.. Nina wasiwasi Wenger akataka kuweka mtu mgumu hapa, kama Chambers, lakini ugomvi wa hawa watu wawili utavutia. Kama Kuna siku ngumu zaidi ambazo Bellerin anaweza kumbana nazo na kuzikumbuka basi ni leo, lakini ni siku ambazo anaweza kuwapa tiketi ya moja kwa moja kwenye mbao Chambers na Debuchy. Kinachoumiza kichwa ni Ile gundi iliyo kwenye viatu vya Hazard, inabidi uwe umeamka vizuri sana kumzuia huyu na wala usiwe mwenye hasira maana maudhi kwake ni kawaida, ndio maana hatumhitaji Chambers wala Debuchy hapo Leo labda Wenger.
Kama Kuna kitu ambacho Arsene Wenger anatakiwa kukiweka kichwani mwa Sanchez na wachezaji wa Arsenal ni Counter Attacks. Hawazijui kabisa, huyu Sanchez anaupenda sana mpira, wale wengine kukaba Counter Attacks hawajui (mkumbuke Oscar, Hazard, Willian eneo hili) hapa ndipo panapoweza kumrudisha Wenger nyuma.
Carzola na Oscar ndo wachezaji wakimya zaidi kuelekea kwenye mchezo huu... (wasiozungumzwa wala kuzungumza). Lakini ubora wa Carzola unahitajika sana kuliko wa huyu mwenzie.. Ile kazi ya kupenya alichokipanga Mourinho golini unahitaji akili ya Carzola, Ozil na Sanchez zifanye kazi kwa Pamoja.
Karata yangu Sasa na wachezaji watakaochanganua mchezo.
Pamoja na yote hayo mchezo utakuwa mguuni kwa Aaron Ramsey. Huyu akicheza vizuri kazi ya Carzola, Ozil itakuwa rahisi sana, na atawafanya Azplicueta na Matic kwa Pamoja wafanye kazi kubwa sana, lakini akishindwa ndipo napoona kifo cha Arsenal kitakapokuwa.
WILLIAN / Oscar
Tofauti na mechi ya Manchester United yeyote Kati ya hawa ubora wake Leo utaamua mchezo huu. Kwangu mimi ningemchukua Willian kwa sababu ya Sanchez. Tatizo la Sanchez katika ukabaji ndilo ambalo litaleta shida kule hasa. Ivanovic + Willian. Maana yangu wakati Arsenal wanamtizama Hazard hili ndilo eneo litakalo leta shida sana. Na hii itampa Hazard nafasi ya kufanya athari katika BLIND SPOT (sehemu isiyofikirika).
Kumkaba Drogba Leo ni rahisi sana lakini pia yeye kuwafunga Arsenal inaweza Kuwa rahisi zaidi. Usishangae kumuona Drogba aliye bora hasa Pamoja na umri wake, hata Torres alitembelea hii tabia kwa Manchester United na Vidic, au Wayne Rooney na wale Aston Villa.
Usisahau ni Wenger Vs Mourinho. Hili nalo ni tatizo wakati Mwingine historia ni mbaya sana na watu wanaishi kulingana nayo. Siwezi kusema matokeo lakini nahisi inaweza Kuwa moja ya siku ambazo Wenger anaweza kucheka lakini kama tu akiweza kutibu COUNTER ATTACKS.
Ningekuwa shabiki wa Arsenal ningewaza COUNTER ATTACKS kuliko Ile defense ya Chelsea. Hapa ndo ubovu wa timu yetu unapolala na ubora wa Chelsea ulipojikita.
Ahsanteni.
By Nicasius Coutinho Suso
Mchambuzi bora wa michezo anayekuja kwa kasi (najiita chipukizi..)
No comments