SOUTHMPTON YAONGEZA PRESHA TOP 4.


Goli pekee la mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane liliwaamsha wapenzi na mashabiki wa Southampton na kuondoa balaa la kuendelea kupotea katika nafasi nne za juu.

Southampton iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Crystsl Palace katika uwanja wao wa nyumbani St. Marys.

Matokeo hayo yanawafanya wafikishe pointi 49 katika msimamo wa Ligi na kupanda mpaka nafasi ya 5 na kuongeza presha kwa timu zilizo juu. Ikiwa ni pointi moja nyuma ya Manchester United wanaokamata nafasi ya 4 na mbili nyuma ya Arsenal walio katika nafasi ya 3.

VILLA PARK:
Wenyeji Aston Villa ikiwa nyumbani Villa Park walichomoka katika balaa la kushuka daraja baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1. Wakiifunga West Brom

Gabriel Agbonlahor alitangulia kuwapa Villa bao la mapema kabla ya Berahino hajaisawazishia West Brom baadae Dakika tatu za majeruhi Christian Benteke aliifungia Villa kwa mkwaju wa Penati na kufanya mchezo huo kuisha kwa ushindi kwa Aston Villa.

Kwa matokeo hayo Aston Villa wanapanda mpaka nafasi ya 17 wakiwa na pointi 25 huku West Brom wakiwa na kocha mpya Tonny Pulis wanabaki na pointi zao 30 katika nafasi ya 13.

KC STADIUM

Katika mchezo mwingine jana Wenyeji Hull City walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Sunderland.
Sunderland wakisawazisha bao kupitis kwa Jack Rodwel.

No comments

Powered by Blogger.