SIMBA YAENDELEZA UBABE KWA YANGA. OKWI AFUNGA GOLI LA MWAKA.
...Na Edo Daniel Chibo
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameendeleza ubabe wake kwa mahasimu zao Yanga baada ya kuwachapa bao 1-0 katika pambano la Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Pambano hilo lililomalizika hivi punde katika dimba la Taifa Jijini Dar Es Salaam lilikua ni la pili msimu huu kwa timu hizo ambazo huteka nyoyo za mashabiki wa soka nchini Tanzania.
Alikua ni Emmanuel Okwi mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyefunga bao ambao linaweza kuwa bao bora kabisa katika Ligi kuu kwa misimu kadhaa.
Goli la Okwi... Ilikua hivi
Ibrahim Ajib akipokea mpira wa Kessy Ramadhani alimtafuta alipo Emmanuel Okwi katikati ya uwanja Okwi akausogeza mbele kidogo huku akilindwa na Mbuyu Twite na Kelvin Yondani kwa mbali kidogo ambao walikua wanamsindikiza tu.Okwi alimwangalia kipa Ali Mustapha aliposimama na kuona mwanya wa kufunga kwani kipa huyo ambaye mara zote hufungwa magoli ya ajabu wanapocheza na Simba alikua amesimama karibu kabisa na kiboksi cha penati ndipo Okwi akaupiga mpira ukilenga lango la Yanga ambalo muda huo lilikua wazi kutokana na kipa kusogea mbele na ndipo mpira ulimpita Kipa Ali Mustapha na Kujaa wavuni akiuangalia asijue la kufanya na kupelekea shangwe kwa mashabiki lukuki wa Simba waliofurika uwanja wa Taifa.
Pongezi nyingi kwa Simba leo ni Uwepo wa Abdi Banda ambaye alikua akicheza kama kiungo mkabaji huyu aliharibu kabisa mipango ya Yanga akitumia umbo lake Refu kuwazidi kete washambuliaji wafupi wa Yanga Ngasa, Msuva na Tambwe.
Katika mchezo wa Leo Haruna Niyonzima wa Yanga alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano akipiga mpira wakati Refa akiwa ameshapuliza filimbi.
Kwa matokeo hayo Yanga wanazidi kuongoza na pointi zao 31 huku Simba wakipanda mpaka nafasi ya 3 wakiwa na pointi 26 pointi 4 nyuma ya Azam wanaokamata nafasi ya Pili na moja mbele ya Kagera wanaokamata nafasi ya 4.
No comments