PELLEGRIN BORA KULIKO MAKOCHA WOTE MWEZI DISEMBA



Kocha wa mabingwa wa ligi kuu nchini England Manchester City, Manuel Pellegrin amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Disemba baada ya kuwabwaga wapinzani wake Arsene Wenger,Jose Mourinho na Luis Van Gaal.
Pellegrin ameibuka kidedea baada ya kupata kura nyingi katika utaratibu wa kupata kocha bora wa mwezi ambao chama cha mpira wa Miguu nchini England wakishirikiana na wadhamini wa Ligi kuu Bank ya Barclays hutoa kula mwezi.



Kocha bora wa mwezi hutokana na matokeo ya timu yake katika mwezi husika na Manuel Pellegrini ameiongoza Manchester City kushinda mechi 5 kati ya mechi 6 walizocheza katika mwezi Disemba.

MICHEZO YA MANCHESTER CITY MWEZI DECEMBER

Sunderland 1-4 Manchester City
Manchester City 1-0 Everton
Leicester 0-1 Manchester City
Manchester City 3-0 Crystal Palace
West Brom 1-3 Manchester City
Manchester City 2-2 Burnley
+++++++++++++++++++


Wakati huo huo Mshambuliaji wa QPR Charlie Austin ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba baada ya kufunga goli 5 ndani ya mwezi huo.

Charlie Austin amewashinda Eden Hazard (Chelsea), Harry Kane (Tottenham), David Silva(Man City), Santiago Carzola (Arsenal) na John Terry (Chelsea)

MAGOLI YA CHARLIE AUSTIN MWEZI DISEMBA

Burnley (W 2-0) - December 6 (1)
West Brom (W 3-2) - December 20 (3)
Arsenal (L 1-2) - December 26 (1)


....Ungana nasi katika
Instagram @wapendasoka
Facebook: wapenda soka-Kandanda
Whatsapp: 0715 127272

No comments

Powered by Blogger.