LIVERPOOL VS CHELSEA HAPATOSHI USIKU WA LEO
Pambano la kombe la Ligi nchini England maarufu kama Capital Cup hatua ya nusu fainali kati ya Liverpool na Chelsea linapigwa leo kuanzia saa 5 kasorobo.
Katika pambano hilo litakalopigwa katika dimba la Anfield jijini Liverpool linazikutanisha timu ambazo zimekua na upinzani mkubwa na kuteka mawazo ya Wapenda soka Duniani.
Liverpool wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 2-0 walioupata ugenini wakiifunga Aston Villa katika Ligi huku Chelsea wao wakiibamiza Swansea City ugenini kwa bao 5-0
Adam Lallana na Nahodha Steven Gerard wanatarajiwa kurudi katika mechi ya leo baad ya kukosekana katika mechi iliyopita dhidi ya Aston Villa
Kwa upande wa Chelsea kipa Thibaut Courtois anaweza kurudi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mechi tatu zilizopita kufuatia maumivu ya kidole wakati Beki Cesar Azpillicueta ataikosa mechi hii kutokana na maumivu ya misuli.
Hili ni kombe lingine ambalo Jose Mourinho amelitolea macho msimu huu kwani bado ana uwezekano wa kushinda makombe yote msimu huu kwakua bado anashiriki katika makombe yote likiwemo Ligi ya mabingwa ulaya,EPL,Kombe la FA na kombe hili la Capital one na hili ndo kombe pekee ambalo uhakika ni mkubwa kwake kuchukua.
Ikumbukwe hili ndo lilikua kombe la kwanza kwa Mourinho wakati alipoanza kuitumikia chelsea wakati huo wakiifunga Liverpool katika fainali bao 3-2

No comments