HIZI BUNDUKI ZA ARSENAL BALAA MAN CITY YALALA 2-0 KWAO


Pengine Arsene Wenger ameanza kupata dawa ya kuzigunga zile timu zinazoitwa kubwa baada ya jana kuachana na mchezo wa kufunguka na kucheza kwa kujihami mwanzo mwisho dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Arsenal kushinda kwa bao 2-0 katika dimba la Etihad zamani likijulikana kama City of Manchester Stadium, Arsenal walicheza kwa tahadhari kubwa wakijua kabisa aina ya wachezaji wa Manchester City.

Goli la kwanza la Arsenal lilipatikana kwa njia ya penati mfungaji akiwa ni Santiago Carzola kwa njia ya Penati baada ya Nacho Monreal kuangushwa na Vicent Kompany na Mwamuzi Mike Deen kuamuru ipigwe penati ambayo ilifungwa na Carzola.

Bao la pili la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud akiunganisha mpira wa Adhabu uliopigwa na Santi Carzola baada ya Sanchez kufanyiwa madhambi na Stevan jovetic.

Kwa matokeo hayo Arsenal wamepanda mpaka nafasi ya 5 wakiwa na pointi 39 pointi 1 nyuma ya Man United wanaokamata nafasi ya 4 na kuwawashia taa nyekundu walio katika Top 4 wakati Man City wanazidi kupata wakati mgumu kutetea ubingwa wao wakiachwa pointi 5 na wanaoongoza Ligi Chelsea wenye pointi 52 ambao mechi ijayo wataikaribisha Man City katika dimba la Stamford Bridge.

Katika mchezo mwingine hiyo jana West Ham waliibamiza Hull City bao 3-0 magoli ya Morgan Amalfitano,Andy Caroll na Stewart Dorwning.

~ Edo Daniel Chibo

No comments

Powered by Blogger.