SOUTHAMPTON VS MAN UNITED ~ HISTORIA INAIPA USHINDI MAN UNITED
Kama Manchester United wataibuka na ushindi leo basi moja ya stori za Wapenda soka inaweza kuwa ni "Tulishajua Southampton hawawezi presha ya kubaki top 4" Vipi kama Southampton watashinda mechi hiyo?
Haya ni baadhi tu ya mambo yanaweza kuongelewa na Wapenda Soka ila ukweli ni kwamba Southampton na Sunderlans wanapitia kipindi kigumu sana hivi sasa kwa kukumbana na timu ambazo mawazo yao ni Ubingwa.
Walianza kwa kufungwa nyumbani na mabingwa watetezi Manchester City badae wakiwa ugenini pale Emiratea waliambulia kichapo tena na leo wako nyumbani kuwakaribisha mashetani wekundu Man United katika dimba la St. Mary.
Kocha wa Southampton Ronald Koeman anaamini kuwa timu yake inaweza kabisa kumaliza katika nafasi nne za juu licha ya kuuza wachezaji wake wengi wakati wa kiangazi.
Manchester United Itaingia katika mchezo wa leo ikiwa imeshinda katika mechi zake mbili zilizopita inakamata nafasi ya 5 pointi moja nyuma ya Southampton.
Chakuvutia zaidi leo ni kukutana tena kwa makocha wa kidachi wanaoziongoza timu hizo ikumbukwe makocha hao yani Luis Van Gaal na Ronald Koeman walishafanya kazi pamoja wakati Luis Van Gaal alipokua kocha wa Barcelona huku Koeman akiwa ni msaidizi wake.
Angel Di Maria ataukosa mchezo wa leo wakati nahodha wa United Wayne Rooney anatarajia kuja.
NAJUWA WAJUA LAKINI........
Mechi za msimu uliopita baina ya timu hizo katika ligi ziliisha kwa sare ya bao 1-1 na katika mechi nane zilizopita baina ya timu hizo,Man United imeshinda zote huku mara 5 zikiwa zimefanyika katika dimba la St. Mary ambalo leo mtanange huo unapigwa.Mara ya mwisho Southampton kuifunga Man United ilikua mwezi Agosti mwaka 2003 Ushindi wa bao 1-0
Katika mechi 3 zilizopita katika ligi Southampton wamefungwa mechi 2 na kutoka sare mara moja wakati Man United imeshinda mechi zake zote 3 zilizopita.
Southampton imechezesha wachezaji 15 ambao walianza katika mechi zao huku Man United ikiwa na wachezaji 26 ambao walianza katika mechi za ligi kuu England msimu huu.
Graziano Pelle ambaye ndiye mkali wa kupachika mabao wa Southampton lakini hajafunga goli lolote katika michezo mitano iliyopita wakati Wayne Rooney ambaye ni Mfungaji wa Manchester United amefunga magoli matano katika mechi 5 za ligi alizocheza dhidi ya Sputhampton
MECHI HII INAANZA MAJIRA YA SAA 5 KAMILI USIKU HUU KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.
No comments