MESSI NA BALAA LAKE APIGA BAO 3 PEKE YAKE BARCA IKIUA 5



Lionel Messi amefunga mabao matatu katika ushindi wa bao 5-1 walioupata Barcelona dhidi ya Espanyol ikiwa ni hat trick yake ya 21 La Liga usiku wa jana.



Wiki haiwezi kuisha salama kama hujawataja hawa watu yani Messi na Ronaldo na wikiend hii tumeweza kuzungumzia stori mbili kali za hawa watu katika ufungaji wa magoli matatu au zaidi kila mmoja.

Wakati Ronaldo alipowafunga Celta Vigo juzi na kuweka Rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick nyingi La Liga kwa kufunga mara 23 Messi jana amefikisha hat trick ya 21 akiwa nyuma ya Ronaldo,Telmo Zarra na Alfredo di Stefano.

Kwa matokeo hayo Barcelona wanasogea mpaka nafasi ya Pili wakiwa na pointi 34 pointi mbili tu nyuma ya wanaoongoza Real Madrid wakati Espanyol wamebaki katika nafasi 12 wakiwa na point zao 14.

Messi alianza kufunga magoli yake dakika ya 45 badae akaongeza la pili dakika ya 50 na hatimaye dakika ya 81 huku magoli mengine ya Barcelona yakifungwa na Gerald Pique na Pedro.

+++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.