LIGI KUU ENGLAND - ARSENAL NA CHELSEA KUKUENDELEZA UBABE UGENINI?



Baada ya mechi za katikati ya wiki kuleta neema kwa timu vigogo katika ligi kuu England, uhondo wa ligi hiyo utaendelea tena leo kwa viwanja 7 kuwa katika wakati mgumu.
Chelsea na Arsenal watakua ugenini kujaribu kuendeleza ushindi katika mechi zao za leo.



Baada ya kuwafunga Totenham bao 3-0 vinara wa ligi hiyo Chelsea watakuwa katika uwanja wa St. James Park kuikabili timu ngumu ya Newcastle ambayo siku za hivi karibuni imefufuka.

Arsenal wao baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakiifunga Southampton katikati ya wiki watasafiri mpaka katika mji wa Stoke kuwakabili Stoke City ambao walipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Manchester United.

Mabingwa watetezi Manchester City baada ya kutoa kichapo kwa Sunderland ugenini leo watakua nyumbani kuwaalika Everton wakikamilisha mechi ngumu zaidi siku ya leo. Everton wataingia katika mechi hiyo baada ya kutoka sare katika mechi iliyopita dhidi ya Hull City.

Sunderland wanaendelea na lile balaa la kukutana na timu ngumu kwa wakati mmoja kwani baada ya kutoka sare na Chelsea baadae kuambulia kichapo dhidi ya Man City leo watakua ugenini kucheza na timu ngumu ya Liverpool.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZOTE ZA LEO EPL

3:45 PM - Newcastle United vs Chelsea
6:00 PM - Hull City vs West Bromwich Albion
6:00 PM - Liverpool vs Sunderland
6:00 PM - Queens Park Rangers vs Burnley
6:00 PM - Stoke City vs Arsenal
6:00 PM - Tottenham Hotspur vs Crystal Palace
8:30 PM - Manchester City vs Everton

NOTE: MUDA NI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI

No comments

Powered by Blogger.