YAYA TOURE AFIKISHA MECHI 100 IVORY COAST


Nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure jana alifikisha mechi yake ya 100 tangu alipoanza kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo maarufu kama Tembo. Yaya Toure alikua akiiongoza Ivory Coast katika kampeni ya kutafuta nafasi ya kucheza katika fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchi Guinea ya Equator kuanzia January 17 mwakani katika mechi dhidi ya Cameroon ambao tayari walishafuzu.




Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana, mashabiki walivamia uwanja baada ya pambano hilo wakishangilia timu yao kufuzu kushiriki kombe la mataifa ya Afrika katika pambano lililopigwa katika jiji la Abdjan nchini Ivory Coast.


Yaya Toure alianza kuichezea timu yake ya taifa mwaka 2004 akiwa katika klabu ya Metalurg Donetsk ya Nchini Ukraine na tangu wakati huo ameweza kuichezea Ivory Coast katika fainali 3 za kombe la dunia yani mwaka 2006,2010 na 2014. Kwa heshima Yaya Toure amezawadiwa fulana iliyoandikwa "YAYA TOURE 100" ambayo alikabidhiwa kabla ya mechi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.