UHOLANZI HALI MBAYA YAKUBALI KICHAPO KINGINE NYUMBANI


Washindi watatu wa Kombe la dunia mwaka huu timu ya Taifa ya Uholanzi imeendelea kusuasua katika mechi zake ikiwa chini ya kocha Guus Hidink baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-2 nyumbani katika dimba la Amstadam dhidi ya timu ya taifa ya Mexico.



Katika mchezo huo ambao Guus Hidink alimweka benchi nahodha na mshambuliaji wa kikosi hicho Robin Van Perse iliduwazwa na soka safi lililochezwa na vijana wadogo wa Mexico ambao walipata mabao yao kupitia kwa Carlos Vella aliyefunga mabao mawili dakika za 8 na 62 Huku Javier Hernandez Chicharito akifunga bao la 3 dakika ya 69.

Uholanzi walipata mabao yao kupitia kwa Viungo Wesley Sneijder dakika ya 49 na Daley Blind dakika ya 74 akipiga shuti la mbali lililomshinda kipa Wa Mexico Guillermo Ochoa.

MATOKEO YA MECHI ZA KIRAFIKI JANA


  • Malaysia 0-3 Syria
  • Uturuki 0-4 Brazil
  • Norway 0-1 Estonia
  • Uholanzi 2-3 Mexico
  • Argentina 2-1 Croatia
  • Belgium 3-1 Iceland

.... Powered by www.facebook.com/wapendasoka-kandanda

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.