PALACE YAPELEKA MSIBA MWINGINE KWA LIVERPOOL
![]() |
| Gayle na Jedinak wafungaji wa mabao ya Palace |
Mapumziko ya wiki mbili kupisha mechi za kimataifa kwa timu za Taifa yameendelea kuleta neema na msiba kwa baadhi ya timu. Kwa upande wa Liverpool ni majanga juu ya majanga baada ya leo kukubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa timu iliyokua katika mstari wa kushuka daraja Crystal Palace.
Iliwachukua dakika mbili tu kwa Liverpool kupata bao la kwanza kupitia kwa Rickie Lambert akipokea pasi toka kwa Adam Lallana na kuwafanya mashabiki wengi wa Liverpool waamini kama leo inaweza kua ndo siku yao ya kucheka baada ya jana Arsenal kulia.
Crystal Palace walitulia na kuweza kuwakabili Vizuri Liverpool wakitumia mashambulizi ya kustukiza juhudi wmbqzo zilizaa matunda dakika ya 17 tu kupitia kwa Dwight Gayle na mpaka mapumziko ikawa ni sare ya 1-1.
Mashuti matatu tu ya Palace katika pambano hilo yalizaa magoli matatu kwa Palace baada ya kupata bao la pili dakika ya 78 kupitia kwa Joseph Ledley na lile la tatu kupitia kwa nahodha Mile Jedinak dakika 3 baadae.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ameonekana kama ameferi mipango yake licha ya usajili mkubwa alioufanya na hajui la kufanya hivi sasa baada ya leo kumweka Benchi Ballotel na mambo bado hayako sawa.
Kwa matokeo hayo sasa Liverpool wamebaki na pointi zao 14 katika nafsi ya 12 wakiwa wameshacheza mechi 12 wakati Palace wao ushindi huo umewapandisha mpaka nafasi ya 16 wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 12 wastani wa pointi moja kila mechi.

No comments