RONALDO VS MESSI LEO OLD TRAFFORD


Ronaldo akiwasili Manchester

Ngome kongwe maarufu kama Old Trafford nyumbani kwa Manchester United leo usiku patakua sehemu maalumu patakapowekwa historia kwa kuwakaribisha wababe katika soka wanaoshindana kwa rekodi Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.



Ronaldo akiwa ndo mchezaji bora wa dunia hivi sasa ataiongoza Timu ya taifa ya Ureno kuwavaa washindi wa pili wa kombe la dunia timu ya taifa ya Argentina inayoongozwa na Lionel Messi.

Mtanange huu wa kimataifa wa kirafiki utapigwa kuanzia majira ya saa tano kasorobo kwa saa za Afrika mashariki.
Messi na Ronaldo wamekua washiriki wakubwa katika tuzo ya mchezaji bora wa dunia tangu mwaka 2008 wakipokezana tuzo hiyo inayoheshimika duniani.
Messi ameshinda mara nne wakati Ronaldo akishinda mara mbili kwa miaka 6 iliyopita.

Ukiacha Messi na Ronaldo kuna mastaa wengine kibao leo kama Angel Di Maria,Sergio Aguero,Carlos Tevez,Pepe,Luis Nani n.k. ambao hao wote wanatarajia kuwepo katika pambano hilo.

No comments

Powered by Blogger.