MTOTO WA DAVID BECKHAM KUKIPIGA ARSENAL
![]() |
| Brooklyn na Tiago Silva |
Brooklyn mwenye miaka 15 amewafurahisha makocha wa Arsenal na kuna mpango wa kumpa mkataba wa muda mrefu wakati atakapofikia miaka 16 mwezi March mwaka 2015 wakati ambao Arsenal wanaweza kumsajili kama mchezaji wa Academy na akifikisha miaka 17 anaweza kusaini kama mchezaji wa kulipwa kutokana na sheria ya soka.
Brooklyn amekua akiwaniwa kwa karibu mno na Klabu za Manchester United na Chelsea lakini ameonekana moyo wake una mapenzi na Arsenal na ameshawahi kufanya mazoezi na Manchester United, Chelsea na Fulham
Sio tu Brooklyn bali hata mdogo wake Romeo David Beckham mwenye miaka 12 ameonekana lulu katika mazoezi ya kikosi cha Arsenal chini ya miaka 13.
![]() |
| Brooklyn,David,Cruz na Romeo(Becks family) |
Beckham na familia yake wanaishi London ambako nyota huyo aliyewika akiwa na Man United,Real Madrid na LA Galaxy ana bonge la mjengo.
+++++++++++++++++++++++++++++++


No comments