MAJANGA - BINGWA MTETEZI NIGERIA YATUPWA NJE KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA.
Nigeria ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imejikuta ikipoteza nafasi ya kushiriki mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 yatakayopigwa nchini Guinea ya Equator baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na Afrika Kusini.
Alikua mshambuliaji Tokelo Rantie wa Afrika kusini ambao wameonekana kuwa bora hivi sasa aliyewapatia vijana hao wa Jacob Zuma bao mbili zote akifunga bao la kwanza dakika ya 42 na la pili dakika ya 48 huku Mshambuliaji Sone Aluko wa Nigeria akirudisha magoli yote mawilli.
Kwa matokeo hayo Nigeria ambao ni mabingwa watetezi sasa wametupwa nje ya mivhuano ijayo ya kombe la mataifa ya Afrika kwani katika kundi A wawakilishi wawili wa kundi hili ni Afrika Kusini iliyokamata nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 12 na Congo iliyokamata nafasi ya Pili ikijikusanyia pointi 10 michuano hiyo
Nigeria imemaliza katika nafasi ya 3 kwa kujikusanyia pointi 8 baada ya michezo 6 ikishinda mechi 2 kutoa sare mechi mbili na kupoteza mechi mbili.

Nigeria walilewa mafanikio ya mda mfupi wanateam nzuri tu ina avarage player sasa sjui nini kime3a cost kiasi hiki.
ReplyDeleteconsistency kwa wachezaji wa kiafrica na team tatizo waliweza Egypt peke yao hii kitu too bad hawakuwa na back up