LIVERPOOL VS CHELSEA MARUDIO YA MACHUNGU YA GERARD
Unaikumbuka ile mechi ya msimu uliopita ambapo ndoto za Steven Gerard kubeba kombe la ubingwa wa England ziliyeyuka baada ya kutoa boko lililotumiwa na Demba Ba kuzamisha ndoto za maelfu ya mashabiki wa Liverpool sio tu uwanjani Anfield bali duniani kote? Pengine hii itakaa katika kumbukumbu za Gerard kulikokitu kingine chochote kwani ilimkosesha nafasi ya kushika lile kombe la ubingwa wa ligi kuu England.
Leo ni marudio ya mechi hiyo baina ya Liverpool ambayo haina msimu mzuri sana tofauti na msimu uliopita wakiwakaribisha Chelsea walio katika kiwango bora kabisa katika uwanja huo huo wa Anfield uliopo katikati ya jiji la Liverpool.
Chelsea ndo vinara wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwa wamecheza mechi 10 na kupata pointi 26 ikiwa ndo timu ambayo haijafungwa mpaka sasa wakati Liverpool wao wanakamata nafasi ya 7 wakiwa wameshacheza mechi 10 na kupata pointi 14 pointi 6 pungufu ya msimu uliopita.
Kwa haraka tu unaweza kuona kuwa Chelsea imepoteza pointi 4 tu katika pointi 30 ambazo walipaswa kuzipata wakati Liverpool wao wamepoteza pointi 16 tangu kuanza msimu huu.
Baada ya kukosa pambano la katikati ya wiki dhidi ya Real Madrid Nahodha Steven Gerard anaweza kuanza leo akiwa na Raheem Sterling, Jordan Henderson,Coutinho, Dejan Lovren na Mario Balotelli huku Daniel Sturadge akiwa bado yuko majeruhi kwa upande wa Wenyeji Liverpool.
Chelsea wao wanafuraha kuwaalika dimbani tena Cesar Azpilicueta,John Obi Mikel, na Loic Remy baada ya kuwa majeruhi wakati Azpilicueta akitumikia kufungiwa mechi 3.
Wakati Liverpool wanafungwa bao 1-0 na Real Madrid katika ligi ya mabingwa ulaya katikati ya wiki Chelsea wao walilazimishwa sare na Maribor katika ligi ya mabingwa pia.
FACTS
- Chelsea imepoteza mechi moja tu katika mechi 6 walizocheza na Liverpool wakishinda mechi 3 na 2 zikiisha kwa sare.
- Chelsea mpaka sasa haijafungwa katika mechi 13 zilizopita katika ligi ikishinda mechi 10 na kutoa sare mechi 3.
- Baada ya ushindi wa bao 2-0 walioupata Chelsea katika mechi dhidi ya Liverpool mwezi April ambapo Chelsea hawakuruhusu bao wameshindwa kuzuia kufungwa bao lolote mpaka sasa licha ya kushinda mechi nyingi.
- Katika mechi 7 zilizopita kwa Liverpool wameshinda mechi 2 tu na Liverpool wamepata pointi chache msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita ambapo baada ya mechi 10 walikua na pointi 20.
MAWAZO YA WAPENDA SOKA
Humphrey (Baba Lincoln)
...... Chelsea wapo katika form ya hali ya juu, kuanzia golini mpaka washambuliaji wao, si Remy, si Costa si Drogba, achilia mbali umri wake.Kwa sababu hiyo, jumlisha rekodi waliyonayo juu ya wapinzani wao kwa siku za hivi karibuni Chelsea wataingia Uwanjani wakiwa vifua mbele...
Liverpool, bado wana majeraha kadhaa, defeat from Newcastle United, plus "Gerrard's slip nightmare are still bad memories that Liverpool will step into the pitch with.."
Kwa misingi hii, tayari Chelsea wana nafasi kubwa ya kushinda, ukizingatia they've yet to loose a game this season...
Waamuzi:
Moja kati ya watu wanao influence matokeo katika epl msimu huu(na mingine huko nyuma) ni waamuzi.
Kuna waamuzi hawako makini kabisa, na ndo wanaoaminiwa katika mechi kubwa, na chama cha soka cha Uingereza, F.A
Mark Cluternburg ambaye alichangia Man United kupoteza mchezo dhidi ya Leicester City katika uwanja wa King Power
Mike Dean, Martin Atkinson na Anthony Taylor, ambaye pia ndo atakuwa Refa wa Game ya leo, umakini au uzembe wake unaweza kuchangia kuamua mshindi katika mechi ya leo, Mechi inaweza kuwa nzuri na ya kuvutia kama tunavyotarajia, au ikaboa kupita maelezo, kama hatokuwa Makini.
Faida ya kucheza nyumbani:
Mpaka sasa Anfield ndo uwanja ambao mashabiki wake wamedhihrisha kuwa mchezaji wa 12 mwenye influence kubwa zaidi ya vilabu vingine pale England, Despite professionalism, Bado mchezaji unaweza kutoka nje ya mchezo kama Atmosphere itakuwa embarrassing, na kuathiri mchezo.
Kwa hiyo kama Liverpool wakitumia vema faida ya kucheza nyumbani, wakiamua...wanaweza kumsimamisha mfalme wa London kwa sasa, ambaye hajafungwa mpaka sasa.
Bahati:
Au uswahilini kwetu tunaita 'ndondokela', hii nayo imo, japo huchangiwa na wachezaji pia kujituma ili kuamua mchezo, so atakayekuwa na bahati leo, ukiachilia mbali mambo mengine, huenda akashinda mchezo, Kati ya Chelsea au Liverpool.
Muda ni Saa 9 na dk 45, leo Mchana
Uwanja, Anfield, Merseyside-Liverpool!
××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments