LIGI KUU TANZANIA BARA - YANGA YAJIULIZA KWA MGAMBO
Baada ya kichapo cha bao 1-0 walichokipata Yanga ugenini kule Kagera leo watakua uwanja wa Taifa Dar es salaam kujiuliza wapi walipokosea watakapoialika timu isiyotabirika ya JKT mgambo katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni.
Yanga itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na pointi 10 katika nafasi ya 4 baada ya kucheza michezo 6 ikishinda mitatu ikitoa sare mmoja dhidi ya watani zao Simba wakati wamepoteza michezo miwili dhidi ya timu zinazotengeneza miwa yani Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.
Yanga pia imeweza kufunga magoli 7 mpaka sasa huku wakiruhusu kufungwa magoli 5.
Kwa Upande wa Mgambo JKT wameshacheza michezo 6 wanakamata nafasi ya 6 wakiwa na pointi 9 sawa na Kagera Sugar. Mgambo wameshinda michezo mitatu kati ya michezo 6 na wameshafungwa mara 3. Wamefunga magoli manne na wameshafungwa magoli matano.
Katika michezo iliyopita Yanga walifungwa bao 1-0 wakati Mgambo waliwafunga Mbeya City bao 2-1 katika dimba la Mkwakwani.
Katika mechi zingine Vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar watawaalika ndugu zao Kagera Sugar katika pambano litakalovurumishwa katika dimba la Manungu katikati ya mashamba ya miwa kule Mkoani Morogoro.
Mabingwa watetezi Azam watakua Chamazi kuwaalika Coastal Union wanaokamata nafasi ya Pili wakiwa na pointi 11 huku Azam wao wakishika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 10.
Washindi wa Pili wa msimu uliopita ambao msimu huu wanaburuza mkia klabu ya Mbeya City imeshawasili Shinyanga kuwakabili Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage.
Polisi Morogoro wanaokamata nafasi ya 12 watakua Jamhuri Morogoro kuwaalika Tanzania Prisons ambao mechi iliyopita walitoka sare ya bao 1-1 na Stand United.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments