LIGI KUU TANZANIA BARA : YANGA NA AZAM ZAAMBULIA VICHAPO HUKU SIMBA IKIENDELEZA SARE



Hatua ya 6 ya Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea jioni hii kwa viwanja kadhaa kuwa katika hali tete.

Mabingwa Watetezi Azam FC wamekubali kichapo cha pili mfululizo toka kwa Wageni wa Ligi Ndanda FC ya Mtwara katika pambano kali lililopigwa katika dimba la Nangwana Sijaona mjini Mtwara.



Bao pekee la Ndanda FC ambayo ilimtimua kocha wake siku za hivi karibuni lilifungwa na Jacob Massawe likiwainua Ndanda FC baada ya kucheza michezo minne bila ushindi.

Huu ni mchezo wa pili Azam anapoteza baada ya ule uliopita kufungwa na JKT Ruvu bao 1-0 licha ya kumaliza msimu uliopita bila kufungwa mchezo wowote wakichukua ubingwa wao wa kwanza katika Historia.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

KUTOKA MOROGORO

Bab Chicharito anaripoti kuwa zimwi la sare limezidi kuwaandama watoto wa msimbazi Simba SC baada ya kulazimishwa sare na Mtibwa Sugar ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Jamhuri Mkoani Morogoro.

Kama ilivyo kawaida ya mechi zilizopita kwa Simba kutangulia kupata bao na hatimaye wapinzani kurudisha ndivyo ilivyokua leo katika mchezo ambao ulikumbwa na upepo mkali kabla haujaanza upepo uliopita uwanjani hapo.

 Simba walipata bao la kuongoza dakika ya 34 kupitia kwa nahodha George Owino kabla ya Mtibwa hawajasawazisha kupitia kwa mchezaji wa Zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Musa Hassan Mgosi ambaye aliuwahi mpira uliomshinda kipa Manyika Peter.

Kitu cha kufurahisha na kutia matumaini ilikua kumwona Kipa chipukizi wa Simba Manyika Peter akidaka penati japokua ilikuja kufunikwa na kushindwa kwake kuzuia kufungwa goli.

Hii ni sare ya 6 sasa kwa Simba ikiwa imeshacheza mechi 6 ikitoka sare mechi zote hizo 6 na kufunga magoli 6 huku ikifungwa magoli 6 pia. Hii inakuja siku chache baada ya kuwasimamisha wachezaji wake watatu Kiemba,Chanongo na Kisiga kwa madai ya kuihujumu timu mara baada ya mchezo uliopita dhidi ya Prisons.

+++++++++++++++++++++++++++++

KUTOKA BUKOBA


Wenyeji Kagera Sugar waliibamiza Yanga kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba mkoani Kagera

Alikua ni Paul Ngway aliyepiga bonge moja la Goli na kuipa Kagera Sugar ushindi mwingine dhidi ya Yanga katika uwanja huo ambao ni mgumu kwa Yanga kupata ushindi.

Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kupoteza mchezo wake wa pili Msimu huu baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Mtibwa Sugar.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO 

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Ndanda FC 1-0 Azam FC
Mtibwa Sugar 1-1 Simba SC
Kagera Sugar 1-0 Yanga SC
Coastal Union 1-0 Ruvu Shooting
JKT Ruvu 1-2 Polisi Morogoro

No comments

Powered by Blogger.