LICHA YA UHOLANZI KUSHINDA 6-0 KOCHA LUIS VAN GAAL ANUNA



Katika watu ambao hawakufurahia ushindi wa jana kwa Uholanzi wakiifunga Latvia bao 6-0 basi ni kocha wa zamani wa Uholanzi akiifundisha Manchester United hivi sasa Luis Van Gaal ambaye mechi hiyo imemuongezea idadi ya majeruhi katika kikosi chake kwa kiungo wake mkabaji Daley Blind kuumia goti.



Blind aliumia dakika ya 20 tu ya mchezo huo uliopigwa katika dimba la Amstadam na nafasi yake kuchukuliwa na Jordy Clasie na kufanya idadi ya majeruhi katika kikosi cha Manchester United wakati huu wa mechi za kimataifa kufikia watatu baada ya Michael Carick na David De Gea kuumia pia.

Uholanzi ilipata magoli yake kupitia kwa nahodha Robin Van Perse aliyefunga bao moja,Arjen Robben magoli mawili, Klas Jan Huntelar magoli mawili na Jeffrey Bruma akifunga bao moja.

Idadi ya wachezaji wa Man United walio Majeruhi mpaka sasa ni  pamoja na Michael Carick, Rafael Da Silva, John Evans, Phil Jones, Marcos Rojo, Radamel Falcao, Ashley Young,David De Gea, Jesse Lingard

MATOKEO YA MECHI ZA JANA

KUNDI A 
Uholanzi 6-0 Latvia
Czech 2-1 Iceland
Uturuki 3-1 Kazakhstan

KUNDI B
Belgium 0-0 Wales
Cyprus 5-0 Andorra
Israel 3-0 Bosnia

KUNDI H
Azerbaijan 0-1 Norway
Bulgaria 1-1 Malta
Italia 1-1 Croatia

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.