ARSENAL VS MAN UNITED - REKODI ZINAIPA MAN UNITED USHINDI



Ni siku nyingine tena miamba ya soka nchini England Arsenal watakapoikaribisha Manchester United katika dimba la Emirates jijini London ikiwa ni mechi ya kwanza msimu huu kwa Manchester United katika mji kuu huo wa Uingereza.
Mechi hiyo itaanza saa 2:30 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki na itachezeshwa na mwamuzi Mike Dean.



+++++++++++++++++++++++++++++++++

HALI ZA TIMU

Kwa upande wa wenyeji Arsenal mshambuliaji wake Olivier Giroud amepona mguu wake uliovunjika miezi kadhaa iliyopita na atakua tayari kuwakabili Manchester United kama kocha atampanga.
Mikel Arteta naye amepona majeruhi ya misuli yaliyokua yanamsumbua lakini Danny Welbeck na Theo Walcot wanaweza kukosa mechi hiyo.

Kwa upande wa wageni Manchester United kiungo Daley Blind na Radamel Falcao wameongeza ile listi ya majeruhi wa United msimu huu lakini taarifa nzuri kwa mashabiki wa United ni kusikia kuwa Luke Shaw,Michael Carick, Angel Di Maria na David De Gea ambao jana walionekana katika mazoezi wanaweza kucheza leo.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

FACTS 

  • Manchester United imepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 14 ambayo imezikutanisha timu hizo katika mashindano yote ikishinda mechi 10 na kupoteza mchezo mmoja huku wakitoka sare mara 3. 
  • Mara ya mwisho Arsenal kuifunga Manchester United ilikua mwezi Mei mwaka 2011 kwa goli 1-0 lililofungwa na Aaron Ramsey.
  • Katika historia timu hizi zimekutana mara 219 katika mashindano yote huku Man United ikishinda mara 92na Arsenal kushinda mara 79 huku wakitoa sare mara 48.
  • Huu ni msimu wa pili Arsenal wakiwa chini ya kocha Arsene Wenger wanapata pointi chache baada ya kucheza michezo 11 wakiwa na pointi 17 tu hivi sasa mara ya kwanza ilikua msimu wa 2012/2013 ilipokua na pointi 16.
  • Alexis Sanchez amefunga magoli 12 katika mechi 14 akiwa na Arsenal msimu huu katika mashindano yote ikiwa ni pamoja na magoli 6 katika mechi mechi 4 zilizopita.
  • Man United haijashinda mechi yoyote ya ugenini katika ligi kuu msimu huu ikitoka sare mara 3 na kupoteza mara 2. Haijashinda ugenini tangu mwezi April mwaka huu walipoifunga Newcastle United.
  • Manchester United inakamata nafasi ya 7 hivi sasa ikiwa na pointi 16 baada ya michezo 11 katika ligi hii ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kwa klabu hiyo kwa miaka 25 mara ya mwisho ilikua mwaka 1989/1990 walipopata pointi 14 katika michezo 11.
  • Juan Mata amefunga magoli manne na kutengeneza mengine mawili katika mechi zote alizocheza dhidi ya Arsenal katika mashindano yote.
  • Wayne Rooney anaungana na Robbie Fowler kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi dhidi ya Arsenal akifunga magoli 10 mpaka sasa.
  • Robin Van Perse amefunga magoli matano katika mechi sita zilizopita kati ya timu hizi,Magoli mawili akiifungia Arsenal na matatu akifungia Man United.

ARSENAL VS MAN UNITED TANGU MWAKA 2009


  • Feb 12, 2014 Arsenal 0-0 Man Utd 
  • Nov 10, 2013 Man Utd 1-0 Arsenal
  •  Apr 28, 2013 Arsenal 1-1 Man Utd 
  • Nov 3, 2012 Man Utd 2-1 Arsenal 
  • Jan 22, 2012 Arsenal 1-2 Man Utd 
  • Aug 28, 2011 Man Utd 8-2 Arsenal 
  • May 1, 2011 Arsenal 1-0 Man Utd 
  • Dec 13, 2010 Man Utd 1-0 Arsenal
  • Jan 31, 2010 Arsenal 1-3 Man Utd
  • Aug 29, 2009 Man Utd 2-1 Arsenal
  • May 16, 2009 Man Utd 0-0 Arsenal



Prepared by Edo Daniel Chibo ( 0715 127272)



++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++





No comments

Powered by Blogger.