ARSENAL HAWANA JIPYA KWA MAN UNITED YACHAPWA 2-1 KWAO
Mazoea ni kama tabia na hiyo ni kama kusema Arsenal wamezoa kufungwa na Man United baada ya kukubali kichapo tena cha bao 2-1 katika uwanja wa Emirates jijini London.
Arsenal ikiwa katika kiwango bora kabisa imeshindwa kupata ushindi na kuishia kupiga mashuti 9 langoni kwa United ambayo hayakua na madhara yoyote zaidi ya kuokolewa na Kipa wa Man United David De Gea.
Man United walionekana kuzidiwa kabisa dakika zote 90 za mchezo huku Arsenal wakitawala kila idara huku Man United wakifanikiwa tu kupeleka mashambulizi langoni mwa Arsenal na katika mashuti mawili ambayo walipiga langoni mwa Arsenal yote yalizaa magoli.
Beki wa Arsenal Kieren Gibbs alijifunga dakika ya 56 wakati akijaribu kuokoa mpira wa Ashley Young aliyeingia kuchukua nafasi ya Luke Shaw ambaye aliumia
Goli la pili la Man United lilipatikana dakika ya 85 baada ya Di Maria kumtengenezea Wayne Rooney ambaye alikimbia na mpira winga ya Kushoto na kumhadaa beki na kipa wa Arsenal na kufunga kiurahisi
Man United wakitumia mfumo wa kupark bus walirudi wote nyuma na kuwafanya Arsenal nao kupanda wote ili kushambulia na hiyo ilileta shida kwa Arsenal kwani Mpira wa kushtukiza ulioanzia kwa Rooney na kupiga pass ndefu iliyomkuta Di Maria bado kidogo izae goli kwani mpira ulipita nje kidogo lango la Arsenal.
Mshambuliaji wa Arsenal aliyeingia kuchukua nafasi ya Aaron Ramsey , Olivier Giroud alifunga bao la kufutia machozi la Arsenal ndani ya dakika 8 za muda wa nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 2-1 ushindi ukienda tena kwa Man United.
Kwa matokeo hayo Man united imefikisha pointi 19 katika nafasi ya 4 huku Arsenal wakibaki na pointi 16 katika nafasi ya 8.
KILICHOTOKEA
● WafungajiGiroud 90+5 (Arsenal)
Gibbs 56' (OG), Rooney 85',(Man United)
● Mashuti yaliyolenga goli
Arsenal 9-2 Man United
● Mashuti yasiyolenga goli
Arsenal 8-7 Man United
● Kona
Arsenal 11-5 Man United
● Umiliki wa Mpira (Possesion)
Arsenal 62%-38% Man United
● Faulo
Arsenal 12-8 Man United
● Offside
Arsenal 1-4 Man United
● Kadi za njano
Arsenal 2-1 Man United
..Powered by www.facebook.com/wapendasoka-kandanda



No comments