AGUERO AENDELEZA MSIBA KWA MAN UNITED




Sergio Kun Aguero ameendeleza ubabe kwa Manchester United baada ya kuiongoza Manchester City kuwafunga Manchester United katika mchezo wa watani wa jadi uliopigwa katika uwanja wa Etihad.

Aguero ameendeleza rekodi ya kuwafunga Man United baada ya kufunga goli dakika ya 63 akiunganisha mpira wa krosi ya Gael Clichy na kuifanya United kupoteza mchezo mwingine ambao pengine mashabiki wake walijua wangeibuka na ushindi baada ya kucheza vizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea.



Balaa lilianza kuwakumba Man United dakika ya 39 baada ya beki wake wa kati Chris Smalling kupata kadi ya pili ya njano baada ya kupata kadi nyingine ya njano dakika 8 kabla hivyo kutolewa kwa kadi nyekundu na kuwafanya United kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu.

Mechi hiyo iliyotawaliwa na ubabe wa hapa na pale ulishuhudia wachezaji watano wakipata kadi za njano watatu wa Man City na wawili kwa upande wa United.

Pigo lingine kwa United lilikua dakika ya 56 baada ya Beki mwingine wa kati Marcos Rojo kutolewa akiwa katika machela kufatia kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick McNair.

Manchester United licha ya kupiga mashuti 8 ni mawili tu yaliyolenga lango la Man City wakati wenyeji Man City walipiga mashuti 11 na 6 kati ya hayo yakilenga lango huku Man City wakimiliki mpira kwa 52% wakati Man United wao walikua na 48% ya umiliki wa mpira.

Kwa matokeo hayo Man City wanasogea katika nafasi ya 3 safari hii wakiwa na pointi 20 wakati Man United wameshuka nafasi moja na sasa wanakamata nafasi ya 9 wakiwa na pointi 13 timu zote hizo zikiwa zimecheza mechi 10.

++++++++++++++++++++++++++++++++++

1 comment:

Powered by Blogger.