ADEBAYOR AMTIMUA MAMA YAKE NA KUMTUHUMU KUWA ANAMPIGA JUJU.


Adebayor na mama yake mzazi

Mshambuliaji wa Totenham Hotspurs na nahodha wa timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor amekana kuwa amemfukuza mama Yake katika jumba lake huko Togo.



Adebayor ambaye makazi yake sasa ni London anakofanya kazi ya kucheza soka katika klabu ya Tottenham inasemekana amemfukuza mama yake mzazi kwa madai kuwa yeye na ndugu zake wanamloga ili asifanikiwe.

Akizungumza na kituo cha redio cha Ghana kinachojulikana kama Peace FM dada wa Adebayor anayeitwa Maggie alimtuhumu Adebayor kwa kushindwa kumpa msaada mama yake na  hajamwona yapata mwaka sasa na zaidi ya yote amemtimua jambo ambalo Adebayor mwenyewe amelikana na kusema ni uzushi kwani mama yake aliondoka kwa mapenzi yake mwenyewe na sio kwa kufukuzwa.

Adebayor ambaye mshahara wake kwa wiki ni paundi 101,000 amemlaumu mama yake kwa kumwombea mabaya kwani anawaambia watu kuwa yeye Emmanuel hatofanikiwa
" Ni kwa vipi naweza kuwa karibu na mama ambaye ndiye anayemwambia kila mtu kuwa sintofanikiwa hivyo ni bora nikabaki mwenyewe na kufanya yangu"
Amewataka ndugu zake kuacha kumpiga juju.

Adebayor mwenye miaka 30 hivi sasa amefunga magoli mawili tu katika mechi 12 msimu huu akiwa na Spurs na Jumapili hii watasafiri ugenini kuwavaa Hull City.

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.