TFF VS WAMILIKI WA VIWANJA = MWIZI ANAYEJARIBU KUIBA NYUMBANI KWA JAMBAZI
:
Asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kwenye mahangaiko yangu ya kukidhi mahitaji ya maisha ya mwili, nasikiliza kipindi cha michezo na Burudani cha moja ya Radio kubwa Nchini inayopatikana Mkoani Mwanza.
Katika kipindi hicho namsikiliza kwa makini meneja wa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine unaopatikana Mkoani Mbeya Bwana Modestus Mwaluka akilalamikia mgawo mdogo wanaopewa na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kuwa ni mdogo.
Anafafanua zaidi Bwana Mwaluka kuwa licha ya viwango vya makusanyo ya viingilio kutofautiana lakini kiwango wanachopewa siku zote ni Tshs. 1,000,000/= katika mgao wa mapato ya Sokoine.
Mwaluka anasema baada ya makusanyo ya mechi ya mzunguko wa kwanza iliyokusanya zaidi ya Shilingi milioni ishirin walipewa mgawo wa shilingi milioni moja tu, mechi ya pili iliyoingiza zaidi ya shilingi milioni thelathini bado mgawo ikiwa ni zile zile shilingi milioni moja.
Pia analalamikia kitendo cha TFF kufanya siri makusanyo ya viingilio mpaka wao wanapojisikia kutangaza mara nyingi ikiwa ni baada ya siku tatu.
"Hii siyo sawa na haikubaliki" anasema meneja huyo wa uwanja unaotumiwa na timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zote za jijini Mbeya.
Nitarudi katika hoja yangu ya msingi baada ya kuangalia namna fedha za viingilio zinavyogawanya kwa vilabu na namna pesa zinavyofyekwa.
Baada ya malalamiko mengi ya vilabu kuhusu makato ya viingilio na mgawo kwa vilabu Serikali na TFF waliahidi kulishughulikia swala hilo.
Hata baada ya kulishuhulikia swala hilo bado kilio kimekuwa pale pale. Vilabu bado vinalalamikia mgawo kidogo wa mapato ya viingilio.
Ilikuwa ni sawa na vichekesho unapotajiwa namna pesa zinavyokatwa na mikondo zinakoelekezwa.
Mfano, wakati tayari zimeshakatwa fedha ya gharama za mchezo bado unajumlishiwa na fedha za kuwalipa waamuzi, au umeshalipa gharama za ulinzi bado pia utadaiwa fedha ya askali polisi waliokuwa lindo siku ya mechi n.k.
Narudi kwenye hoja ya uzi huu.
TFF baada ya kuvinyonya sana vilabu kwa kushirikiana na baadhi ya watu serikalini na baadhi ya wamiliki wa viwanja, sasa wana wanajaribu kuwakwapulia wamiliki wa viwanja ambao wanaonekana ni wajanja kwa maswala kama ya kuuzunguka mbuyu zaidi ya TFF wenyewe.
Nasema haya baada ya kuangalia wengi wa wamiliki wa viwanja hivyo ni kina nani.
Zaidi ya asilimia tisini (90% ) ya viwanja vinavyotumika hapa nchini vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) japo sijui uhalali wa umiliki wao ni halali au la.
Ni nani wa kuumia kama kila mmoja ataamua kutumia ujeuri wake kati ya CCM na TFF?
Hapa natafakari Paka anavyotaka kulazimisha kumuona Chui kama anavyomuona Panya. Pia najaribu kuona mwizi anavyohangaika kumpora jambazi na kunifanya nicheke na kuipitisha siku kwa kichekesho rahisi namna hii.
Nasubiri kusikia na kuona mengi ikiwa ni pamoja na mpango wa Shirikisho la soka kutaka kuvikata vilabu kiasi fulani cha asilimia za fedha za udhamini na hili la wamiliki wa viwanja vya mpira wa miguu nchini kuanza kulalamikia mgawo wa fedha za viingilio.
Imeandaliwa na Abel Sichembe <> member: Wapenda Soka.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments