SOKA LA BONGO ~ MGUU WAKO NDIYO PESA ZAKO
Utumwa wa fedha ni mzuri sana katika dunia ya leo ambapo kila mtu anaweza kusujudu na kufanya shughuli yeyote ile bila kujali ili mradi aipate, ona vijana wa afrika wanavyo ifikiria ulaya ila juhudi na maarifa vina tukwamisha na adhabu yake ni kali kuliko ile ya kupigwa mawe. Miaka ya nyuma nilikua nipo uwanjani ninatafuta sarafu yangu ya shillingi ishirini niliyo idondosha wakati tukifanya mazoezi kwa ajili ya mechi mwalimu wangu Ndumbaro akaniuliza nini kinanisumbua nikamwambia kilicho nikuta alinipa jibu ambalo nilishindwa kulifanyia kazi mpaka leo. Alisema "Your foot is your money go and get it" sikutilia maanani kwakua niliamini ninacho kifanya nikujifurahisha tu na nikibahatisha nikacheze Lipuli basi na niliamini mpira upo pale na kweli enzi zile unamwambia nini mtu wa iringa na mwalimu Ndumbaro kuhusu Lipuli wasikufurahie lakini kwa bahati mbaya Lipuli ipo migombani sasa hoi.
Wanasoka wa Tanzania wa sasa wamekua wanafanya soka ni sanaa wakiamini walipo ndio mahala sahihi kwao hawana cha kuwaza kua mguu wake ndio sayari ya maendeleao na ni njia halali ya safari ya mafanikio huku soka wameliacha kwa uhuru wa Samata.
Hivi kuna mchezaji hata moja wa Tanzania aliwahi kumuuliza Ally Mayay alikua ana ingiza kiasi gani wakati anasakakata kabumbu alikua analala vip wakati kambi ya timu ya Taifa ni ajabu na inaweza sikitisha. Leo hii mchezaji hata asipo lipwa miez sita wala hawezi kulalamika kwa kua yeye mwenyewe haoni thamani yake na hajui kazi yake kama ni ya muhimu katika timu kazi yake ni kutupa nafasi ya kuona mitindo tu na kumcheki akiwa anagombea chips kama msanii chipukizi wakati yeye ni mchezaji tena wa haja lakini anakua tu msanii anacheza anavyotaka hajali kitu.
Kila mtu ni msanii watendaji ni wasani makocha ni wasanii nani bora hapo , hapo bora ataibuka kua Okwi ambaye yeye hana sanaa anawaza pesa tu kwakua utumwa wake ni mzuri wala hatumii nguvu anajua watakuja tu na cheki zao za pesa na atachukua tu na kuwaacha wakipiga kelele kama mlevi alie kunywa pombe kali na kumshutumu mkewe kamzimia taa wakati bado ina waka. Hii ni kutokana na sanaa tuliyo kua nayo sijaamini kua nchi yetu ya Tanzania haina akina Okwi na makocha hawawezi kuwa na uwezo wa kutengeneza akina Okwi wenye njaa ya uhuru wa soka la samata.
Kila siku ni siku ya faraja ya tabibu yeye ana mipango mingi ya kutibu na kutengeneza utamu wa soka kuliko sanaa lakini kakwama na shibe ya wachezaji anaamini watanzania hawawezi kupambana hawawezi kufanya yale watanzania wanataka kuona yanapatikana viwanjani.
Bora nirudi kijijini ndio kauli zetu kumbe kule tuliacha angalau cha kutumia imekua fasheni isiyo kua natija hapa nchini kwa vilabu vyetu kunyang’anyana wachezaji bila sababu na kulaumiana kua wanahujumiana hivi tuna umakini kweli we unataka ucheze soka la kimataifa alafu huandai wachezaji wa kukupigania kwanini usiangalie na kuwavuruga majirani ili upate mchezaji.
Na mwangalia Samata na uUimwengu huko waliko hua najiuliza wao ni watu waliotoka nchi gani kwani huko waliko wana sifika kwa yale wafanyayo uwanjani na utulivu wao mwisho wasiku utumwa wana unapata jina zuri la ukijituma utashinda ukilala utanenenepa kazi wanapiga pesa wakati tegete anakula mkeka pale Yanga na wala hashtuki anaamini sanaa yake pale Yanga ina mlipa zaidi ya akina ulimwengu.
Tanzania na nchi nyingine za Africa hatuna tofauti kubwa sana lakini zipo ni Watanzania tu wasio na Hamu wao nikawaida tu kila kitu kilivyo ni sawa sasa hii imeingia hadi kwenye mifupa na miguu ya wachezaji wao wanaamini ni bora waendelee kuitafuta sarafu iliyo dondoka na kumuacha Okwi, Jaja, Coutinho na Niyonzima wakivaa jezi zenye maandishi ya your foot is your money go and get it wakimaanisha miguu yako ndio pesa za zako nenda kazichukue ndio wanachukua unalalamika nini mnyime pasi atatafuta na atapiga goli mita ishirini na atapiga mpira mzuri akina sisi tuata mpigia shangwe na tuna mwongeza pesa wakati we mtanzania una sanaa na soka umeliacha kwenye ulimwengu wa samata.
Naam ni dakika ya ngapi hii hivi okwi yupo sawa tutashinda tu hii mechi jiulize swali kwanini asiuliziwe singano ambae amebebeshwa jina zito la Messi abadilishe matokeo hii yo ni sana makocha ni wana sanaa hawawezi kumfanya singano akawa kiwanda cha mabao katika kila mechi anayo cheza wao wata kuja na mistali ile ile ahh anapiga chenga nyingi mnno apunguze kwanini wewe mwalimu usimfundishe kutumia chenga hizo kutengeneza mabao au huangalii ulaya wewe ukamuona Rahim Sterling akikusanya watu na kuwatupa kule nakunamwona kwenye kibendela wenzie wamemzingira wakishangilia bao.
Tuamke mie nimeamka……
Imeandaliwa na
lucas_tz 0764665151
(Lucas Kifyasi) wapenda soka

No comments