LIGI KUU TANZANIA BARA: SIMBA BAADA YA KUTOKA POLISI LEO IKO STENDI.



Hatua ya tatu ya ligi kuu nchini Tanzania maarufu kama ligi kuu ya Vodacom itaendelea leo kwa viwanja vitano kuwa katika wakati mgumu.
Mabingwa watetezi Azam FC wamesafiri mpaka Mbeya kuwavaa Prisons ya huko.

Azam FC itaingia katika mchezo wa leo ikiwa inaongoza ikiwa na pointi 6 ikiwa imeshacheza michezo miwili ikishinda yote huku ikiwa imeshafunga magoli matano manne kati ya hayo yakifungwa na Didier Kavumbagu ambaye amesajiliwa na Azam akitokea Yanga.
Kwa upande wao Prisons wanakamata nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi wakiwa wameshacheza michezo 2 wakishinda moja na kufungwa mmoja.



Katika Uwanja wa Taifa Simba baada kutoka sare na Polisi Morogoro watawakaribisha wageni wa ligi hiyo klabu ya Stendi United toka Shinyanga.
Simba wakiwa wameshacheza michezo miwili hawajashinda hata mmoja wakitoka sare michezo yote miwili wanakamata nafasi ya 10 wakati Stendi wao wanakamata nafasi ya 9.

WANAOONGOZA KWA UFUNGAJI
Didier Kavumbagu - Azam FC (Magoli 4)
Ame Ally - Mtibwa Sugar (Magoli 2 )
Ally Mrisho - Mtibwa Sugar (Magoli 2)

MSIMAMO WA LIGI

RATIBA KAMILI

Polisi Morogoro vs Kagera Sugar
Coastal Union vs Ndanda FC
Simba SC vs Stand United
Prisons vs Azam FC
Ruvu Shooting vs Mbeya City

NOTE: Mechi zote zitaanza saa 10 jioni

No comments

Powered by Blogger.