HABARI 8 KALI ZA SOKA ASUBUHI YA LEO


NYUMBANI ( TANZANIA)


1. Mbwana Samata ataikosa mechi ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania na Benin baada ya kuumia akiwa na klabu yake ya TP Mazembe lakini Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto na Juma Luzio wanaocheza nje ya nchi watakuwepo.

2.  Kocha wa zamani wa Azam FC Muingereza Stewart John Hall amesema anaamini kuwa Yanga itaifunga Simba katika mchezo wa tarehe 18 mwezi huu kwakua ni timu inayofundishwa na kocha bora mwenye hadhi na kiwango cha kuifundisha klabu kubwa kama Yanga.



3.  Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Musa Hassan Mgosi amesema kilichomkimbiza Simba ni chuki majungu na unafiki wa baadhi ya watu wanaodhani Simba ni Yao.
Mgosi mfungaji wa bao la kwanza la Mtibwa dhidi ya Yanga katika mechi ya Ufunguzi anaamini yeye bado ni mchezaji mzuri na atazidi kulithibitisha hilo uwanjani lengo kuu kwake kwa sasa ni kuisaidia Mtibwa kushinda ubingwa wa Ligi ya Tanzania.

4. Timu ya Stendi United ya shinyanga inakabiliwa na adhabu ya faini ya laki 3 kufuatia kukataa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa imani za kishirikina katika mchezo wake dhidi ya Simba ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1.



ULAYA

5. Luke Shaw ataiwakilisha timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 baada ya ile ya wakubwa kutokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya kocha Roy Hudgson na Southgate ambaye anaifundisha timu ya Taifa chini ya miaka 21.
Ikumbukwe timu zote hizi zinasaka nafasi ya kushiriki fainali za Ulaya.

6. Kocha wa Real Madrid Carlo Ancellot anaamini hakuna mtu wa kumzuia mshambuliaji wa timu yake Cristiano Ronaldo kubeba tena tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka huu.
Ronaldo juzi alipiga hat trick ya 3 msimu huu ikiwa ni ya 22 tangu alipotua La Liga mwaka 2009 akitokea Manchester United.

7.  Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anaamini winga wake Raheem Sterling atasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo licha ya tetesi zilizozagaa kuwaniwa na Real Madrid na PSG.
Raheem anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Liverpool mkataba ambao pengine utamwongezea mshahara na kumshawishi kubaki Klabuni hapo kwani kwa sasa analipwa paundi 50,000 kwa wiki na kuna tetesi ambazo Wapenda Soka tumezipata katika mkataba mpya atapewa paundi kuanzia 100,000 mpaka 150,000.

8. Solomon Kalou ameonekana kufurahia maisha ya soka la Ujerumani akiwa na klabu ya Hertha Berlin aliyojiunga nayo akitokea Lile ya Ufaransa.
Kalou mwenye miaka 29 ambaye ameshafunga magoli matatu katika mechi 5 za Bundesliga anaamini ataipa mafanikio Hertha Msimu huu kwakua wameonekana kumwamini.

... Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo
{ 0715 12 7272 }

No comments

Powered by Blogger.