ALIYEWASHINDWA TAIFA STARS AWAPIGA MAN UNITED BONGE LA GOLI
Hali ilikua tete kwa Manchester United jana usiku baada ya kupigana japo kupata sare na kufanikiwa kusawazisha dakika za lala salama na kufanya matokeo kuwa 2-2 katika pambano la ligi kuu England dhidi ya West Bromwich Albion
Man United iliyokua ikihitaji pointi 3 jana kurudi katika nne bora (top 4) ilijikuta ikitafuta japo sare kujinusuru na balaa la kufungwa.
Alikua ni kiungo na nahodha wa Benin Stephan Sessignon ambaye wiki iliyopita Timu yake ya Taifa ilikubali kipigo cha bao 4-1 toka kwa Taifa Stars aliyefunga bonge moja la goli akiunganisha krosi ya chinichini ya beki wa Wes Brom Wisdom.
Man United walizinduka baada ya Maroune Fellain aliyeingia kuchukua nafasi ya Ander Herrera kupiga shuti kali na kuandika bao la kusawazisha la United ikiwa ni dakika chache tangu kuanza kwa kipindi cha pili.
Ubovu wa safu ya Ulinzi ya United ambayo jana ilikua ikiongozwa na Phil Jones na Marcos Rojo ilikubali kumruhusu mshambuliaji raia wa Uingereza akiwa amezaliwa Burundi Saido Berahino kuandika bao la pili kwa Wes brom na kumfanya chipukizi huyo kuongoza katika listi ya wafungaji bora wa ligi msimu huu ambao ni raia wa England akiwa na magoli 6 mpaka sasa.
Dakika 6 za mwisho ilishuhudiwa Man United ambayo imekua ikizoeleka enzi za Sir Alex Ferguson kwa kucheza kwa nguvu dakika za mwisho baada ya kulazimisha na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Delay Blind huku United ikishambulia kwa kasi na nguvu huku Ashley Young aliyeingia kuchukua nafasi ya Angel Di Maria kuonekana yuko vizuri baada ya kutoka majeruhi.
West Brom wao walionekana wako vizuri muda wote wa mchezo huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza huku Brunt wa West Brom akiibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
TATHMINI YA MCHEZO
- Jumla ya mashuti 8 yalipigwa na Wes Brom mawili kati ya hayo yakilenga goli na 6 yakitoka nje huku United wakipiga mashuti 22, 7 kati ya hayo yakilenga goli na 14 yakitoka nje ya goli.
- Wes Brom walipiga pasi 356 na Man United wao wakipiga pasi 574
- United wakimiliki mpira zaidi kwa 63% huku West Brom wakimiliki kwa 37%
- Man United ilipata kona 11 wakati West Brom wao hawakupata kona yoyote
××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××
No comments