YANGA YATAKATA TAIFA. CONTINHO NA MSUVA MASHUJAA



Yanga SC vijana wa Jangwani wamezinduka na kuitandika Prisons ya Mbeya kwa 2-1 katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa Jijini.

Ikiwa na Kumbukumbu mbaya Ya kufungwa na Mtibwa katika mechi ya ufunguzi Yanga iliingiza "silaha" zake zote wakiwemo Wabrazil Jaja na Continho na kuweza kuutawala vilivyo mchezo huo hasa kipindi cha kwanza. Huku Continho akitangulia kuipatia Yanga bao kwa shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliopita ukuta wa Prison na kumshinda kipa wa timu hiyo na kujaa wavuni.
Hivyo mpaka mapumziko Yanga walikua mbele kwa bao hilo moja huku mchezaji mmoja wa Prison akitolewa kwa kadi nyekundu kufatia kumfanyia madhambi Ngasa.



Kipindi cha pili Prisons ambao mchezo uliopita walishinda Ruvu Shooting pale Mabatini Pwani walionekana wako vizuri zaidi licha ya kuwa pungufu na kuweza kusawazisha bao dakika ya 67 kufatia mpira wa krosi uliomkuta mfungaji wa bao hilo Ibrahim Hassan lakini Yanga walisawazisha dakika moja baadae kupitia kwa Simon Msuva ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Continho.

   ■■■■■■■■TATHIMINI YA MCHEZO ■■■■

●  MASHUTI YALIYOLENGA GOLI
.. Yanga walipiga mashuti 6 golini wakati Prisons wao wakipiga mashuti manne golini.

● MASHUTI YALIYOTOKA NJE YA GOLI
.. Yanga na Prisons kila timu ilitumia nafasi walizopata huku kila timu ikipiga mashuti manne yaliyotoka nje ya lango.

● KONA
.. Yanga walipata kona 9 wakati Prisons wao walipata kona 4.

● FAULO
.. Prisons ilionekana kufanya faulo nyingi kwani mpaka mchezo unamalizika walikua wamefanya faulo 15 wakati Yanga walifanya faulo 12.

● UMILIKI WA MPIRA
..Kwa ufupi mpira ulikua umebalance licha ya Prisons kuwa pungufu lakini takwimu zinaelekeza kuwa Yanga walimiliki mpira kwa 51% wakati Prisons wao walikua na 49%.

                ◇◇◇◇◇◇◇ JKT RUVU 0-2 KAGERA SUGAR ◇◇◇◇◇◇◇◇◇

Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex , JKT Ruvu wameangukia pua baada ya kubamizwa bao 2-0 na Kagera Sugar.

Magoli ya Kagera Sugar yalifungwa na Salum Kanoni na Rashid mandawa katika mchezo huo ambao ulikua wa kushambuliana muda wote wa mchezo.
Ikumbukwe Kagera Sugar walipoteza mchezo wao uliopita walipofungwa 1-0 na Mgambo jijini Tanga wakati JKT Ruvu walitoka sare na Mbeya City jijini Mbeya.

{Edo Daniel Chibo}

No comments

Powered by Blogger.