MUIMBAJI MAARUFU WA INJILI ATOA YA MOYONI KWA VIONGOZI WA SIMBA,YANGA NA TFF
Mwimbaji Ambwene akiwa na mwandishi wa habari hii ndugu Allen Kaijage |
Wakati mechi ya Simba na Coastal Union ikiendelea pembeni ya
kiti changu alikua ameketi muimbaji maarufu wa nyimbo za injili,naye si
mwingine ni Ambwene Mwasongwe. Wengi wao wanamfahanu Ambwene Mwasongwe kama
muimbaji ila haufahamu Maisha yake ya upande mwingine kama mshabiki na
mkereketwa wa mpira wa miguu.
Najua una shauku ya kujua nini Ambwene Mwasongwe, mwimbaji wa wimbo wa 'misuli ya imani'
anakifahamu kuhusu mpira wa miguu,
basi fuatilia mahojiano haya.
Mwandishi: Ambwene habari yako?
Ambwene: Safi habari yako
Mwandishi: Nimefurahi kukuona hapa leo, Ambwene wewe ni
mshabiki wa timu gani?
Ambwene: Kwa Tanzania naipenda sana Simba ila ulaya mimi ni
mshabiki wa kutupwa wa Chelsea.
Mwandishi: Umeanza kuipenda Simba lini?
Ambwene: Miaka ya 92
Mwandishi: Wachezaji gani wa Simba wa zamani ambao walikua
wanakuvutia?
Ambwene: Dua Said, Abdallah Kibaden na Edward Chumillah.
Mwandishi: Wachezaji gani wa simba wa sasa wanaokuvutia?
Ambwene: Kiukweli navutiwa sana na Uhuru Seleman, pia Okwi na
Kiemba.
Mwandishi: Umeanza kuipenda lini Chelsea?
Ambwene:Tangu 1997 Enzi za kina Gullit, FLO na Dennis Wise
Mwandishi: Ulishawai kucheza mpira?
Ambwene: Nimecheza sana ila miundombinu ilinikwamisha
nisisonge mbele
Mwandishi: Miundombinu kama ipi?
Ambwene: Viwanja na vifaa vya michezo
Mwandishi: Una lolote la kuwaambia viongozi wa mpira wa
miguu Tanzania?
Ambwene:Ninayo mengi sana ila kikubwa nawaomba viongozi wa
simba, yanga na TFF waendeshe soka kwa ukweli na uwazi. Unajua viongozi wetu
wengi si wa kweli ndio maana timu zetu kongwe hazifanikiwi. Pia na hata TFF kutokuwa
wa kweli kunafanya timu yetu ya Taifa isisonge mbele
Mwandishi: Ambwene ahsante
Ambwene: Karibu
No comments