MIWANI PANA YA EDO ~ KUELEKEA MICHEZO YA LEO KATIKA SOKA   


*ENGLAND - EPL
Mechi kubwa inayotazamwa na wengi leo ni kati ya Arsenal na Manchester City ikipigwa katika dimba la Emirates kuanzia saa 9 kasorobo mchana.
Hapa tutakumbushia mchezo wa ngao ya hisani mwezi mmoja uliopita ambapo timu hizi zilikutana na Man City wakakubali kichapo cha bao 3-0

Huu utakua mchezo wa kwanza kwa Bakary Sagna kucheza dhidi ya Arsenal baada ya kuhama mwanzoni mwa msimu. Pia mchezo wa kwanza kwa Danny Welbeck ambaye uhamisho wake akitokea Manchester United umezua gumzo wengi wakiilaumu United kumwachia.

Man city inakamata nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi kuu Nchini England wakiwa na pointi 6 wakati Arsenal wako katika nafsi ya 7 wakiwa na pointi 5 wote wakicheza michezo mitatu mpaka sasa.

UTABIRI WANGU
ARSENAL 1-2 MAN CITY



RATIBA KAMILI
14:45  : Arsenal vs Manchester City
17:00 :  Chelsea vs Swansea City
17:00 :  Crystal Palace vs Burnley
17:00 :  Southampton vs Newcastle United
17:00 :   Stoke City vs Leicester City
17:00 :   Sunderland vs Tottenham Hotspur
17:00 :   West Bromwich Albion vs Everton
19:30 :   Liverpool vs Aston Villa

*SPAIN - LA LIGA

Hii ni wikiend nzuri mno kuangalia mechi za Ligi kuu nchini Hispania kwani kuna mechi mbili kali ambazo kama kweli unapenda soka huwezi kuzikosa.
Mechi ya kwanza kati ya Barcelona na Athletic Bilbao ni mechi ambayo natarajia kuona ushindani mkubwa kwajili ambavyo Bilbao imejengwa upya na kocha Ernesto Valverde.
Athletic Bilbao inakamata nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi ikiwa imecheza mechi 2 imeshinda moja na kutoa sare 1.
Pia ikiwatumia wachezaji wake wajanja uwanjani Iker Muniain,Ibai Gomez na Aymeric Laporte wanaweza kubadili sura ya mchezo muda wowote huku wakitumia pasi fupi fupi zilizowashinda Napoli katika ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa upande wa Barcelona itakua mechi ya kwanza msimu huu kuwaona Neymar na Messi wakicheza pamoja wakiwa chini ya kocha mpya Luis Enrique.
Barcelona inayokamata usukani kwakua timu pekee katika msimamo wa ligi ambayo imeshinda mechi zote mbili ilizocheza ikiwa na pointi 6.

UTABIRI WANGU
Barcelona 3-1 Athletic Bilbao

REAL MADRID vs ATHLETICO MADRID

Timu kutoka jiji la Madrid Real Madrid na Athletico Madrid wanakutana katika Madrid dabi pambano linalotarajia kuanza mida ya saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ikipigwa katika dimba la Santiago Bernabeu
Hii si mechi ya kukosa kwani kwa siku za karibuni imezikutanisha timu hizi mara nyingi kwa kipindi kifupi. Athletico Madrid ya sasa ambayo inanolewa na kocha Diego Simeone imekua mwiba mchungu kwa Real kwani ilishazoeleka kwa miaka 13 iliyopita Athletico Madrid hawakuwa kushinda wanapocheza na Real Madrid lakini baada ya kuja huyu jamaa kibao kimebadilika.
Msimu uliopita Athletico waliweza kupata pointi 4 katika michezo miwili ya ligi na kuchukua ubingwa wa La Liga
Yaweza kua mechi ya kwanza kwa Javier Hernandez Chicharito akiwa na Real Madrid tangu alipohamia Real akitokea Man united.

UTABIRI WANGU
REAL MADRID 2-2 ATHLETICO MADRID

RATIBA KAMILI

17:00: Barcelona vs Athletic Bilbao
17:00: Malaga vs Levante
21:00: Real Madrid vs Atletico Madrid
23:00: Celta Vigo vs Real Sociedad

*GERMAN- Bundesliga

Bundesliga inaaanza kuchanganya sasa japo mechi kubwa hazijaanza kuchezwa ila ni wikiend nzuri ambayo unaweza ukatulia na kuona jinsi wachezaji wapya waliosajiliwa na vilabu vikubwa wakifanya mambo.
Xabi Alonso akitokea Real Madrid anaweza kucheza leo akiwa na uzi wa FC Bayern Munich wakati Shinji Kagawa akirudi Dortmund pengine anaweza kuanza leo baada ya Marco Reus kuwa majeruhi watakapocheza na SC Freiburg nyumbani Signal Induna Park.

RATIBA KAMILI

16:30 : Bayern Munich vs VfB Stuttgart
16:30 : Borussia Dortmund vs SC Freiburg
16:30 : Hertha Berlin vs Mainz
16:30 : SC Paderborn 07 vs FC Cologne
16:30 : TSG Hoffenheim vs VfL Wolfsburg
19:30 : Borussia Monchengladbach vs Schalke 04

MECHI ZINGINE LEO

*ITALIA - Serie A

19:00 : Empoli vs AS Roma
21:45 : Juventus vs Udinese

*French Ligue 1

18:00 : Stade Rennes vs Paris Saint-Germain
21:00 : Bastia vs Lens
21:00 : Montpellier vs Lorient
21:00 : Nice vs Metz
21:00 : St Etienne vs Cae
21:00 : Stade de Reims vs Toulouse

Tukutane baada ya mechi hizi kuona nini kilitokea

..... Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo
Waweza nipata whatssap kwa 0762427272
facebook: wapenda soka-kandanda
Instagram: edodanielchibo

+++++++++++++++++++++++++++++++++×××+×××××××××××××++××

No comments

Powered by Blogger.